October 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Vituo vya utayari vyaongeza wanafunzi mashuleni

Wanafunzi wakijisomea

Spread the love

MPANGO wa Kuboresha Elimu Tanzania kwa shule za msingi (EQUIPT TANZANIA) kwa kuanzia vituo vya utayari umechangia kwa kiasi kikubwa wanafunzi kuongezeka mashuleni, anaandika Dany Tibason.

Mbali na vituo vya utayari kuongeza idadi kubwa ya wanafunzi kujiunga na darasa la kwanza kwa wingi pia shule nyingi zimeongeza ufaulu kutokana na mipamgo mbalimbali ambayo EQUIPIT TANZANIA  inaifanya katika kujenga mahusiano mema kati ya walimu, wanafunzi na wazazi.

Mwalimu wa kituo cha utayari cha Lionii kilichopo Bahi Sokoni wilaya ya Bahi mkoani Dodoma, Tutusi Msemakweli amesema kitendo cha kuwepo kwa vituo vya utayari vimechangia zaidi watoto wanaojiunga na darasa la kwanza kuongezeka.

Amesema ni jambo la kawaida katika maeneo ambayo yana jamii ya watu wafugaji kutokuwa na mwamko wa watoto wao kushindwa kujiunga katika shule za msingi lakini kutokana na kuanzishwa kwa vituo vya utayari watoto wengi wa jamii ya kifugaji wameweza kujiunga na darasa la kwanza.

Mwalimu Msemakweli akizungumza na waandishi ambao walitembelea kituo hicho alisema ni kazi kubwa kuwapata watoto wengi wanaotoka katika jamii ya wafugaji lakini kutokana na EQUIPT TANZANIA  kutoa mbinu mbalimbali za ufindishaji kwa walimu wa vituo vya utayari imekuwa rahisi kuwapata wanafunzi wengi ambao ili kuwa ngumu kuwapata.

Akizungumzia mbinu ambazo wanazitumia walimu hao kuwafundishia watoto hao wa vituo vya utayari alisema ni kuimba, kucheza, kuangalia picha mbalimbali za kuvutia pamoja na kuimba nyimbo ambazo zinajenga uelewa kwa wanafunzi.

Alisema kitendo cha kuwepo kwa vituo vya utayari pia jamii imeweza kufunguka na kutambua umuhimu wa elimu kwa watoto wao na kupelekea jamii kujitolea kutoa nafaka kwa ajili ya kusaga unga kwa lengo la kuwapatia chakula na uji watoto wao.

Kwa upande wake mwalimu wa darasa la kwanza katika shule ya msingi ya Bahi Sokoni alisema kitendo cha kuanzishwa kwa mradi wa kuwepo kwa vituo vya utayari kumechangia kwa kiasi kikubwa kuongezeka kwa wanafunzi ambao wanajiunga darasa la kwanza  huku watoto hao wakiwa na ujasiri na ari ya kupenda masomo.

Alisema licha ya kuwa EQUIPT TANZANIA ni mradi ambao unafadhiliwa na Serikali ya Uingereza huku hukisimaniwa na serikali kupitia Wizara ya Elimu, na kusisitiza kuwa iwapo mradi huo ukikoma ni jambo jema serikali ikaendeleza kuwepo kwa vituo vya utayari ambavyo vimeonekana kuwa kivutio kikubwa cha elimu.

error: Content is protected !!