
Spread the love
WATANZANIA wameshauriwa kutumia bidhaa zenye nembo ya Shirika la Viwango Tanzania (TBS), ili kuepukana na utitiri wa vyakula vinavyozalishwa bila viwango kwa matumizi ya mlaji, anaandika Dany Tibason.
Ushauri huo umetolewa na meneja wa kampuni ya Chef Asili Co. LTD mkoani Dodoma, Lupyana Chegula, alipokuwa akitoa mafunzo kwa wafanyakazi wa kampuni hiyo kuhusiana na bidhaa zinazotegenezwa ambazo hazina viwango.
Aidha, amewataka wafanyakazi kufanya kazi zao kwa bidii na kwa ubunifu, ili waendane na kasi iliyopo ya serikali ya awamu ya tano ambayo imekuwa ikisisitiza kila Mtanzania kuwajibika kwenye eneo lake.
More Stories
Mapadri 25, Masista 60 waaga dunia Tanzania
TCRA yajitosa bei za vifurushi
Huawei yaunga mkono malengo endelevu UN