MAHAKAMA ya Wilaya ya Dodoma imepiga kalenda kesi ya Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea (Chadema) hadi Septemba 4 mwaka huu kutokana na uchunguzi wa kesi hiyo kutokamilika, anaandika Dany Tibason.
Kubenea anashtakiwa kwa kosa la jinai ambalo anadaiwa kumshambulia mbunge wa viti maalum (CCM), Juliana Shonza wakati wa bunge la bajeti.
Hakimu James Karayemaha alipanga tarehe hiyo na wakili wa serikali Phobie Magili, alikubaliana naye hivyo kesi hiyo itaendelea Septemba 4, mwaka huu.
Awali Kubenea alisema utaratibu wa kisheria uliotumika siyo mzuri hivyo ni vyema kesi hiyo ingebaki polisi hadi hapo upepelezi utakapokamilika na kwamba ni matumizi mabaya ya rasilmali za serikali.
Naye wakili anayemtetea mshitakiwa Kubenea, Isaac Mwaipopo amesema kuwa wao bado wanasubiria upelelezi ukamilike kwani wana imani na mahakama.
Leave a comment