May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wamiliki wa nyumba, ardhi ‘wakaidi’ kukiona

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula

Spread the love

 

WIZARA ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, imeielekeza Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga kuanza kuchukua hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kutuma ilani ya ubatilisho kwa wamiliki wa nyumba. Anaripoti Nasra Bakari, DMC … (endelea).

Kauli hiyo imetolewa leo Jumatano, tarehe 12 Mei 2021, bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk. Angeline Mabula wakati akijibu swali la Dunstan Kitandula, Mbunge wa Mkinga.

“Je, ni lini serikali itafuta hati ya mashamba yaliyotekelezwa kwa zaidi ya miaka 20 wilayani Mkinga hususani shamba la kwamtii ili ardhi hiyo igawiwe kwa wananchi,” amehoji Kitandula.

Akijibu swali hiyo, Waziri Mabula amejibu amesema, kwa mujibu wa sheria ya ardhi (sura 113), kila mmiliki anapaswa kuendeleza ardhi aliyomilikishwa kwa kuzingatia masharti yaliyosainishwa katika nyaraka za umiliki.

Amesema, kwa wamiliki wanaobainika kukiuka masharti ya umiliki, sheria hiyo imeelekeza hatua mbalimbali za kuchukua ikiwemo kubatilisha milki husika.

“Ni kweli kuwa mashamba yenye umiliki za hati na. 14501 (ekari 2841) na 4722 (ekari 58), kwamtii wilayani Mkinga yanayomilikiwa na kampuni ya kwamtii Estate Ltd kwa matumizi ya kilimo yana ukiukwaji wa masharti ya umiliki.

“Hata hivyo imebainika kuwa katika daftari la kumbukumbu la msajili wa hati, hatimiliki za mashamba hayo zimewekwa rehani kwa kukopewa fedha na hivyo kuwa na third part interest,” amesema Mkinga.

Mkinga amesema, mara baada ya milki za mashamba hayo kubatilishwa, hatua za kuyapanga, kuyapima na kuyakanyaga upya kulingana na mahitaji halisi ya sasa zitaendelea.

error: Content is protected !!