Thursday , 30 March 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Ulaya yafadhili kiwanja cha ndege Sumbawanga
Habari Mchanganyiko

Ulaya yafadhili kiwanja cha ndege Sumbawanga

Spread the love

 

SERIKALI ya Tanzania, imejikita katika kukamilisha ujenzi wa kiwanja cha ndege cha Sumbawanga kilichopo mkoani Rukwa. Anaripoti Nasra Bakari, DMC … (endelea).

Hayo yamesemwa leo Jumatano, tarehe 12 Mei 2021, bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mwita Waitara, wakati akijibu swali la Mbunge wa Kalambo, Josephat Kandege.

“Je, mpango wa serikali wa ujenzi wa uwanja wa ndege eneo la Kisumba wilayani Kalambo, umefikia hatua gani kwa sasa?” ameuliza Kandege.

Waitara amesema, miongoni mwa viwanja vinne vilivyofanyiwa upembuzi yakinifu na usanifu wa kina na kupata ufadhili kutoka Benki ya Uwekezaji ya Ulaya (EIB), ni kiwanja cha ndege cha Sumbawanga, Rukwa.

Mwita Waitara, Naibu wa Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi

Amesema, aidha serikali imekamilisha taratibu za kupata mkandarasi na kupewa idhini kutoka EIB, kinachosubiriwa ni kupata fedha baada ya taratibu za kimkataba kukamilika.

“Baada ya kukamilisha ujenzi wa viwanja vya ndege vya mikoa vilivyosalia ikiwemo Sumbawanga, serikali itaendelea na ujenzi wa viwanja vingine vidogo kwa hadhi ya airstrip ikiwa ni pamoja na kiwanja cha ndege cha Kalambo.

“Napenda kuwashauri wananchi wa Kalambo kutumia kiwanja cha ndege cha Sumbawanga mara ujenzi wake utakapokamilika,” amesema Waitara.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

NMB Bonge la Mpango – ‘Moto Uleule’ yazinduliwa, Milioni 180…

Spread the loveMSIMU wa tatu wa Kampeni ya kuhamasisha utamaduni wa Kuweka...

Habari Mchanganyiko

Rais Samia awataka wahariri kufanya kazi bila uoga, upendeleo

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan amewataka wahariri wa vyombo...

Habari Mchanganyiko

STAMICO yasaini mkataba wa bilioni 55.2 kuchoronga miamba GGML

Spread the loveSHIRIKA la Madini la Taifa (STAMICO) limezidi kufanya vizuri katika...

Habari Mchanganyiko

NMB yatoa traksuti za Mwenge wa Uhuru Mtwara

Spread the loveBENKI ya NMB imetoa traksuti kwa mkoa wa Mtwara ambako...

error: Content is protected !!