February 26, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Wafugaji tuhumani kuwapiga watoto chapa kama mnyama

Spread the love

RIPOTI ya Haki za Binadamu na Biashara imetaja kupungua vitendo vya Ukatili wa kupigwa chapa ya moto kama mnyama kwa watoto mkoani Geita. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Ripoti hiyo iliyoandaliwa na Kituo cha Sheria na Haki za Binaadamu LHRC imezinduliwa rasmi leo tarehe 16 Agosti 2018.

Akiizungumzia Ripoti hiyo Mkurugenzi wa Kituo hiko Anna Henga amesema kuwa kituo hiko kilibaini matendo ya ukatili dhidi ya watoto kwenye mkoa wa Geita ambapo watoto wenye kutumikishwa kwenye kuchunga mifugo walipigwa chapa ya moto sambasamba na wanyama wanaowachunga.

Ameesema kuwa kituo hiko kilikemea na kutoa elimu kwa jamii ya maeneo hayo ambapo matokeo ya elimu hiyo ni kupungua kwa kiwango kikubwa cha ukatili huo.

Tito Magoti Wakili wa kituo hiko ameleza kuwa LHRC ilipambana kuhakikisha ukatilii huo unakoma kwenye Mkoa wa Geita.

Amesema kuwa utafiti wao ulibaini kuwa hapa nchi vitendo hivyo vipo kwenye jamii ya wafugaji Mkoani Geita ambapo watoto wanatumikishwa kuchunga wanyama kama vile Ng’ombe na Mbuzi nao wanapigwa chapa ya Moto kama wanavyopigwa wanyama hao.

error: Content is protected !!