Monday , 26 February 2024
Home Habari Mchanganyiko Professa Mbarawa aagiza kukusanywa kodi
Habari Mchanganyiko

Professa Mbarawa aagiza kukusanywa kodi

Spread the love

WAZIRI wa Maji na Umwagiliaji Professa Makame Mbarawa ameiagiza Mamlaka ya Maji na Umwagiliaji mkoani Mwanza (MWAUWASA) kuongeza jitihada za ukusaji wa kodi kutoka Sh. 2.2 bilioni kwa mwezi hadi bilioni 2.8. Anaripoti Moses Mseti, Mwanza … (endelea).

Mbarawa amesema endapo mamlaka hiyo itaongeza jitahada za ukusaji wa kodi kwa kasi itasaidia pia kuwaunganishia wananchi maji kwa haraka zaidi.

Kauli hiyo ameitoa jana wakati wa ufunguzi rasmi wa jengo jipya la ofisi za mamlaka hiyo lililojengwa kwa kiasi cha Sh. 7 bilioni, ufunguzi ambao ulikwenda sambamba na uzinduzi wa mita za malipo ya maji kabla (luku ya maji) jijini Mwanza.

Mbarawa ameitaka mamlaka hiyo kuhakikisha kuanzia Septemba mwaka huu ukusanyaji wa mapato uanzie kiasi cha Sh. 2.8 bilioni kwa mwezi kwa kuwa wananchi wengi wana nia ya kutumia maji safi na salama hivyo ni jukumu lao la kukusanya kodi.

“Mamlaka nyingi ukusaji wao wa fedha unasuasua lakini nyie (Mwauwasa) nimeona mnajitahidi sana kufanya kazi nilikuja hapa niongee vitu vikali ila mmenifurahisha baada ya kuona jengo lenu ni kubwa na zuri sana.

“Ukiangalia mamlaka nyingine kama Arusha nilikuta wanakusanya kiasi cha Sh. 1.2 bilioni sasa nimewambia wakusanye Sh.  1.8 bilioni, Moshi wao walikuwa Sh. 600 milioni na sasa ni nimewaambia Sh. 900 milioni,” amesema Mbarawa.

Pia amesema mamlaka hizo ni lazima zihakikishe zinafikia kwa haraka malengo yao ya ukusanyaji wa fedha hatua ambayo itasaidia kuleta mabadiliko ya kiutendaji na kuleta tija.

Professa Mbarawa amesema ndani ya mamlaka hizo kumekuwepo na vishoka wengi ambao wanawaunganishia maji wananchi kinyume na utaratibu na kuwataka kuacha mara moja kwa kuwa inachangia kuikosesha serikali fedha nyingi.

Hata hivyo, aliwaomba wafantakazi na watendaji wa juu wa mamlaka hiyo kuongeza kasi ya kuwaunganishia maji wananchi kwa kuwa maji ni uhai.

Katika hatua nyingine Professa Mbarawa amesema kuhusu matumizi ya mita za malipo kabla itasaidia kuondoa malalamiko ya wananchi waliokuwa wakilipa fedha kubwa ikilinganishwa na matumizi ya maji.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella amesema kama viongozi watahakikisha wanaendelea kuunga mkono jitihada zinazofanywa na mamlaka hiyo ili kuleta maendeleo kwa Taifa.

Mkurugenzi wa mamlaka ya maji na Umwagiliaji Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Antony Sanga, amesema lengo lao ni kuhakikisha wanawaunganishia wananchi maji ili kutimiza wajibu wao.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

RC Geita awafunda wahitimu wapya GGML

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Geita, Martine Shigela ametoa wito kwa...

Habari Mchanganyiko

Biteko asisitiza umuhimu wa EREA sekta ya nishati

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari Mchanganyiko

Tembo aongoza migongano binadamu, wanyamapori

Spread the loveIMEELEZWA kuwa asilimia 80 ya migongano baina ya binadamu na...

Habari Mchanganyiko

“Watanzania tembeleeni vivutio vya utalii”

Spread the loveSHIRIKA la Hifadhi za Taifa (TANAPA) limewataka Watanzania kujitokeza kutembelea...

error: Content is protected !!