September 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wakulima Dodoma wadai kucheleweshewa fidia

Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Godwin Kunambi

Spread the love

WAKULIMA zaidi ya 70 wa kata ya Mtumba jijini Dodoma ambao maeneo ya yalipimwa na ofisi ya jiji bila kushirikishwa wanadai kitendo cha kucheleweshewa fidia zao kinawarudisha nyuma kimaendeleo. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Mwenyekiti wa kamati ya kudai haki ya maeneo hayo, Ayubu Sanga amesema pamoja na maeneo yao yalipimwa bila wa kupewa taarifa, lakini walikubaliana walipwe fidia, cha kushajgaza hadi sasa hawajalipwa.

Amesema Oktoba 2018 ofisi ya jiji iliwaambia wananachi hao kuwa hadi kufikia Desemba mwaka jana watakuwa wamelipwa fedha hizo huku wakiambiwa watalipwa kiasi cha sh 1.5 milioni kwa hekari.

Sanga alisema kuanzia kipindi hicho hadi sasa hakuna hata mwananchi mmoja aliyelipwa fedha hizo, huku akitumia nafasi hiyo kumuomba mkurugenzi wa jiji la Dodoma, Godwin Kunambi na ofisi yake kuwalipa fedha hizo ili waweze kufanya shughuli za maendeleo.

“Kata ya wananchi hao zaidi ya sabini wapo kwenye hekari 10 na wengine wanazaidi ya hekari 10, na kila hekari moja tuliambiwa tutalipwa shilingi 1.5 milioni,” alisema Sanga.

Akizungumzia malalamiko hayo afisa uhusiano wa wa jiji la Dodoma, Denis Gondwe alisema suala hilo atalifuatialia katika mamlaka husika na pindi litakapokamilika atatoa taarifa.

error: Content is protected !!