Saturday , 3 June 2023
Home Habari Mchanganyiko Dk. Mahenge: Kupandisha bei hakutawasaidia
Habari Mchanganyiko

Dk. Mahenge: Kupandisha bei hakutawasaidia

Spread the love

MKUU wa mkoa wa Dodoma, Dk. Binilith Mahenge amewataka wafanyabiashara wa Dodoma kufanya biashara zao kwa malengo ya kujiongezea kipato kwa njia harari badala ya kupandisha bei ya bidhaa wanazouza. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Kwa Niaba ya Mkuu wa Mkoa, Diwani wa kata ya Matumbulu, Emmanuel Chibago alisema kuwa mkuu wa mkoa amemtuma ili kuweza kuwashauri wafanyabiashara hao waweze kutambua yakuwa uuzaji wa bidhaa ni sehemu ya kutoa huduma na siyo kuwakomoa walaji kwa kuwapandishia bei.

Diwani huyo alikutanana wafanyabiashara wa soko kuu la majengo kwenye mkutano wao mkuu wa kikatiba uliofanyika jijini Dodoma.

Akizungumza kwenye mkutano huo aliwataka wafanyabishara hao kufanya biashara zao kwa malengo ya kujiletea kipato kitakachowawezesha kujipatia mikopo, badala ya kuelekeza kwenye mtizamo ya kupandisha bei mazao yao.

Alisema pamoja na wafanyabiashara kuwa na changamoto mbalimbali zinazowakabili bado Serikali kwa kupitia halmashauri ya Jiji tayari imeanza kutoa fedha  kwa ajili ya ukarabati kwenye baadhi ya maeneo ambayo miundombinu imeharibika na kupoteza hadhi ya kusababisha soko hilo.

“Serikali inatambua changamoto zilizopo kwenu  wafanyabishara wa masoko yaliyopo ndani ya jiji hili, lakini hata hivyo tayari hatua zimeanza kuchukuliwa ikiwa na pamoja na ukarabati ulioanza kwenye soko kuu hili la Majengo kwa upanuaji wa paa ambayo yalikuwa yakivuja,” amesema Chibago.

Awali akisoma risala kwa mkuu huyo wa mkoa wa Dodoma, Mwenyekiti wa soko kuu la Majengo, Hamisi Bomu alisema kuwa pamoja na malengo waliyokuwanayo ya kutaka kujiinua kiuchumi kwa kupitia biashara bado wana changamoto zinazowafanya kutofikia hatua mzuri.

Alitaja changamoto hizo ni pamoja na kuvuja  kwa paa la soko, uwepo wa mkataba usio shirikishi kwa upande mmoja, miundombinu mibovu, eneo lililotengwa la stockyard kutokuwa na kivuli, vifaa vya usafi vichache ikiwa na pamoja na uwepo wa biashara holela pembezoni mwa soko.

Alisema soko hilo limekuwa likihudumia zaidi ya watu 8000 na kuwezesha halmashauri kukusanya mamilioni  ya fedha kwa mwezi yanayotokana na ushuru, lakini bado ahadi za utatuzi na marekebisho ya kasoro hizo umekuwa mgumu.

Hata hivyo pamoja na changamoto iliyopo uongozi wa soko utaendelea kuwaunganisha wafanyabishara kuwa wamoja katika kutafuta maslahi yao na maendeleo na kutafuta sauti moja ya mawasiliano kati yetu na halmashauri ya jiji na taasisi za kiserikali na kiraia kwa ajili ya kufikia malengo ya kukuza mitaji inayotokana na vyanzo vya mapato yetu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Magunia 731 ya bangi yakamatwa, mamia ya hekari yateketezwa Arumeru

Spread the love  MAMIA ya magunia ya madawa ya kulevya aina ya...

Habari MchanganyikoTangulizi

Bosi NIC apandishwa kizimbani, akabiliwa na mashitaka 365

Spread the love  ALIYEKUWA Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bima la Taifa...

Habari Mchanganyiko

Serikali yakabidhi eneo la mahakama ya Afrika ya haki za binadamu

Spread the loveSerikali kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa...

Habari Mchanganyiko

Udhamini wa NMB mikutano ya ALAT wafikia 1.2 bilioni

Spread the loveBENKI ya NMB imeendelea kufanya kazi kwa karibu na Asasi...

error: Content is protected !!