Friday , 2 June 2023
Home Habari Mchanganyiko Kibonde azikwa makaburi ya Kinondoni, huzuni, simanzi vyatawala
Habari Mchanganyiko

Kibonde azikwa makaburi ya Kinondoni, huzuni, simanzi vyatawala

Spread the love

HATIMAYE safari ya mwisho ya aliyekuwa Mtangazaji Mahiri wa  Clouds Media Group, Ephraim Kibonde imemalizika katika Makaburi ya Kinondoni  jijini Dar es Salaam ambapo mamia ya watu ikiwemo viongozi wa kiserikali , wanasiasa na wasanii wamejitokeza kumzika mwanahabari huyo. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Mwili wa Kibonde ulizikwa karibu na kaburi la mkewe marehemu Sara Kibonde,  leo tarehe 9 Machi 2019 majira ya kumi Alasiri .

Viongozi walioshiriki mazishi ya marehemu Kibonde ni pamoja na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dk. Jakaya Kikwete, Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Suleiman Jafo na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Zanzibar, Salum Mwalim, ni miongoni mwa wanasiasa waliojitokeza kumzika Mtangazaji huyo aliyetamba katika kipindi cha Jahazi kinachorushwa na kituo cha redio cha Clouds FM.

Kabla ya mwili wa Kibonde kupumzishwa kwenye nyumba yake ya milele, aliagwa nyumbani kwao maeneo ya Mbezi Africana.

Kibonde alifariki dunia Alfajiri ya tarehe 7 Machi 2019 akiwa njiani kuelekea Hospitali ya Rufaa ya Bugando jijini Mwanza kwa ajili ya kufanyiwa matibabu baada ya kusumbuliwa na presha.

Kibonde alianza kusumbuliwa na presha alipokuwa wilayani Bukoba mkoani Kagera kwenye msiba wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalisha wa Clouds Media Group, marehemu Ruge Mutahaba.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Bosi NIC apandishwa kizimbani, akabiliwa na mashitaka 365

Spread the love  ALIYEKUWA Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bima la Taifa...

Habari Mchanganyiko

Serikali yakabidhi eneo la mahakama ya Afrika ya haki za binadamu

Spread the loveSerikali kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa...

Habari Mchanganyiko

Udhamini wa NMB mikutano ya ALAT wafikia 1.2 bilioni

Spread the loveBENKI ya NMB imeendelea kufanya kazi kwa karibu na Asasi...

Habari Mchanganyiko

Dk. Gwajima atoa maelekezo kwa maofisa maendeleo nchini

Spread the love  WAZIRI wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia Watoto,...

error: Content is protected !!