Saturday , 27 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Wakristo duniani washerehekea Sikukuu ya Krismasi
Habari MchanganyikoTangulizi

Wakristo duniani washerehekea Sikukuu ya Krismasi

Spread the love

Shamrashamra za Krismasi zinaendelea  duniani kote leo Jumatatu, siku ambayo Wakiristo wanasherehekea sikukuu ya kuzaliwa kwa Mwokozi wao Yesu Kristo.

Sikukuu hii imejiri wakati dunia ikielekeza macho yake katika vita vinavyoendelea kati ya Israel na kundi la wanamgambo la Hamas kutoka Palestina,  katika Ukanda wa Gaza na maeneo mengine ya Palestina. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Wakristo duniani kote wanamiminika makanisani leo kuadhimisha sikukuu hiyo ya Krismasi.

Kulingana na imani ya Kikristo, Krismasi ni sikukuu ambayo wanaamini kuwa Yesu Kristo (Isa) alizaliwa bethlehemu nchini israeli.  Wakiristo wanaamini kuwa kuzaliwa kwa Yesu Kristo kuliwaletea ukombozi.

Tarehe 25 mwezi Desemba kila mwaka, Wakiristo kote duniani hutumia siku hiyo kwenda makanisani na baadaye kusherehekea pamoja nyumbani na maeneo mengine kwa kula vyakula na kutoa zawadi.

Mjini Bethlehem uliopo nchini Israel ni mji ambao Wakiristo wanaamini kuwa Yesu alizaliwa huko.

Mwaka huu hakukushuhudiwa shamrashamra kama miaka ya nyuma kutokana na vita vinavyoendelea kati ya Israel na Hamas, huku wengine wakiendelea kuandamana kwa kutaka ndugu zao wanaoshikilia na kuli hili la wanamgambo wa Hamas waachiliwe mara moja na Israel ikomeshe vita vyake dhidi ya raia wa Palestina.

Tayari Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis, alishatoa tamko la kutaka mapigano kati ya Irael na Hamas yasitishwe haraka iwezekanavyo.

“Mioyo yetu, jioni ya leo, iko Bethlehemu, ambapo mkuu wa amani bado anakataliwa na hoja isiyofaa ya vita, na mapigano ambayo, hata leo, yanamzuia kupata nafasi duniani,” amesema Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniai Papa Francis kutoka Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican.

Takriban waumini 6,500, kwa mujibu wa Vatican, wamehudhuria misa iliyoongozwa na papa mbele ya viongozi wa kidini na wanadiplomasia, huku mamia ya wengine wakiifuata kwenye skrini kubwa zilizowekwa nje ya uwanja huo.

Makao makuu ya Ukristo, mji wa Bethlehem – ambapo Kristo alizaliwa kulingana na mila – iliachwa na mahujaji mwaka huu na kufuta sherehe nyingi za Krismasi kutokana na vita.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Jacob, Malisa waachiwa kwa masharti

Spread the love  JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

Habari Mchanganyiko

Polisi wakanusha kufanya uzembe ajali iliyouwa mwandishi Ayo Tv

Spread the loveJESHI la Polisi limekanusha tuhuma zilizoibuliwa dhidi yake  kwamba limekawia...

Habari Mchanganyiko

Rais Samia kuzindua gazeti litakalotoa habari za wafanyakazi Tanzania

Spread the loveSHIRIKISHO la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), liko mbioni kufufua...

error: Content is protected !!