Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Wakazi Mbeya washinikiza Mwabukusi, Slaa waachiwe huru
Habari za SiasaTangulizi

Wakazi Mbeya washinikiza Mwabukusi, Slaa waachiwe huru

Wakili Boniface Mwabukusi
Spread the love

BAADHI ya wakazi wa jijini Mbeya wamepaza sauti zao kwa serikali na kuiomba iwaachie huru au kuwafikisha mahakamani Wakili Boniface Mwabukusi, Mpaluka Said Nyagari maarufu ‘Mdude’ pamoja na Dk. Wilbroad Slaa. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Watatu hao wamekamatwa wiki iliyopita kwa nyakati tofauti na jeshi la polisi nchini ambalo limekiri kuwashikilia kwa ajili ya mahojiano kutokana na tuhuma za kutoa maneno ya uchochezi dhidi ya Serikali.

Wakizungumza na waandishi wa habari hii leo Jumanne jijini humo, mmoja wa wananchi hao Nicodem Mwambigija, amebainisha kuwa mfumo wa haki jinai uliozinduliwa hivi karibuni uliweka wazi kuwa polisi wanapaswa kuchunguza kwanza ndio wakamate watuhumiwa, lakini hali ni tofauti jinsi walivyofanya sasa.

“Nimesikitishwa na taarifa za kukamatawa Mwabukusi na wenzake, kamati ya haki jinai imetamka hivi karibuni kwamba polisi wachunguze kwanza ndipo wamkamate mtuhumiwa.

“Leo ni zaidi ya siku tatu toka walivyokamatwa hawajafikishwa mahakamani, huu mtindo wa kukamata ndio wapeleleze unaumiza watu au namna nyingine inaonekana kama kumuadhibu mtu,” alisema Mwambigija.

Aidha, alisema kitendo cha kuendelea kuwashikilia Mwabukusi na wenzake kwa sababu wameikosoa serikali kwenye mkataba wa uwekezaji katika bandari  Dar es Salaam ni ukiukwaji wa haki za binadamu.

“Sababu ya wenzetu hawa kuukosoa mkataba huu ni kutokana nay a mikataba ya aina hii kwani mwanzo waliuza mashirika ya umma na kutuaminisha kwamba maisha yatakuwa mazuri, lakini hatukuona manufaa yake.

“Sasa umekuja uwekezaji huu wa bandari tuna wasiwasi kwamba tutapa shida zilezile, na baadhi ya uwekezaji wametuletea shida kwa sababu tunasikia ndege zetu zinakamatwa kwa sababu mikataba haikuwa sawa,” aliongozea Mwananchi huyo

Mwabukusi na Mdude walikamatwa usiku wa kuamkia tarehe 12 Agosti, 2023 Mikumi mkoani Morogoro, wakitokea jijini Mbeya walipokwenda kwa ajili ya hukumu ya shauri la kupinga mkataba wa DP World ulioamuliwa kwenye Mahakama Kuu kanda ya Mbeya.

Kwa upande wa Balozi Dk. Slaa, alikamatwa siku ya Jumapili mchana, tarehe 13 Agosti 2023 nyumbani kwake Mbweni jijini Dar es Salaam.

Katika hatua nyingine mmoja wa wanachi ambaye jina lake halikufahamika, alitoa neno kwa kuwatia moyo, huku akiwakumbusha baadhi ya maandikio kwenye kitabu cha Biblia na kutoa mifano mbalimbali na kusisitiza kuwa wasife moyo.

“Kwa wale wanaoshikiliwa na polisi wasife moyo, wawe majasiri, kazi wanayoifanya ni Mungu amewatuma na Mungu huyu katika kitabu cha Nabii Isaya sura ya 41:10-13 anasema usiogope, usifadhaike, uwe na moyo wa ushujaa mimi nitakuwa pamoja na wewe.

“Pamoja na mazimgira waliyonayo waamini Mungu yupo pamoja nao, kama vile Mungu alivyokuwa pamoja na Yusuph alivyokuwa amewekwa gerezani alipokuwa na kesi ya kubambikiwa, ni kama ambavyo Paul na Asila walivyowekwa gerezani baada ya kusema ukweli kuhusu kufufuka kwa Yesu Kristo,” alisema mwananchi huyo.

Mdude Nyagali

Kuhusu watuhumiwa hao kutoa maneno ya uchochezi, mwanchi huyo alisema haoni tatizo bali anaamini walikuwa wakitoa maoni yao, kama hawajasema ukweli wawapeleke mahakamani kuliko kuwashikilia.

“Sioni tatizo mimi naona alikuwa anatoa maoni yake sasa waiangalie ile hoja kama ya kweli. Kama kakosea hajasema kweli ndio maana mahakama zipo. Basi wangemchukua kumpeleka mahakamani kuliko hiki kinachofanyika sasa.

“Sitetei wahalifu na kama mtu amekosea mahakama zipo, nakumbuka DPP alimshtaki Mwabukusi kwenye Kamati ya Maadili ya Mawakili Tanganyika, hata kwa kukamatwa kwake kumezuia Mwabukusi asiende kujitetea, Je huo ndio utaratibu na haki?” aliuliza mwananchi huyo.

Hayo yanajiri ikiwa zimetimia siku ya nne tangu watatu hao wakamatwe na jeshi la polisi huku Dk. Slaa na Mdude ambao wamegoma kutoa maelezo ya awali kwa mujibu wa mawaikili wao, inadaiwa kuwa huenda mashtaka yakabadilika na kusomewa kesi ya uhaini ambayo haina dhamana.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za SiasaTangulizi

Samia awataka watanzania kudumisha muungano

Spread the loveRais wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan amewataka Watanzania kuendeleza Muungano kwa...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

error: Content is protected !!