Saturday , 27 April 2024
Home Kitengo Biashara Wafanyabiashara waitwa Bandari ya Dar es Salaam
BiasharaTangulizi

Wafanyabiashara waitwa Bandari ya Dar es Salaam

Spread the love

 

WAFANYABIASHARA wametakiwa kutumia Bandari ya Dar es Salaam, kusafirisha mizigo yao badala ya kutumia bandari za mbali, ili kuokoa muda na gharama. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Wito huo umetolewa leo Ijumaa, tarehe 4 Agosti 2023 na Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam, Mrisho Selemani Mrisho, akizindua huduma mpya ya usafirishaji mizigo kutoka bandari hiyo kwenda maeneo mbalimbali nje ya nchi, inayotolewa na Kampuni ya PMM Shipping Limited, kupitia meli yake kubwa ya Mv. Mirembe Judith.

“Kwa sasa hivi mizigo ya Zanzibar inashushwa Mombasa kisha inapakiwa kwenye meli ndogo kwenda Zanzibar , kwa nini tuwanufaishe wenzetu? Mombasa na Zanzibar ni mbali inachukua zaidi ya saa 10, lakini hapa kwenda Zanzibar saa hazizidi tano. Inatakiwa waje hapa kuna meli kubwa sasa ya Mv. Mirembe itapeleka mizigo yao kwa wakati huko na kwa gharama nafuu,” amesema Mrisho.

Mrisho amesema kuwa, awali wafanyabiashara walikuwa wanapata changamoto ya mizigo yao kuchelewa kutolewa bandarini na kukumbana na adha ya ongezeko la gharama, kutokana na kukosekana kwa meli kubwa inayokidhi kuisafirisha kwa wakati mmoja.

Amesema changamoto hiyo kwa sasa imeanza kutatuliwa, baada ya wawekezaji kuanza kuleta meli kubwa za mizigo, ikiwemo Mv. Mirembe Judith, ambayo inasafirisha mizigo kutoka Bandari ya Dar es Salaam, kuelekea maeneo mbalimbali ikiwemo Zanzibar, visiswa vya Comoro, Mombasa, Durban nchini Afrika Kusini.

Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam, Mrisho Selemani Mrisho

“Tulikuwa na mazungumzo marefu na wamiliki wa Mv. Mirembe Judith hatimaye wameweza kuja, kama mnavyofahamu kuna meli kubwa zinabeba mizigo zinaleta Bandari ya Dar es Salaam, ambayo makasha kati ya 1,000 hadi 2,000 yanapaswa kwenda Zanzibar, hivyo kulikuwa na changamoto ya meli ndogo kwenda huko kwa wakati kisha gharama zinakuwa kubwa,” amesema Mrisho.

Naye Mkuu wa Operesheni wa Kmapuni ya Express Chartaring and Shipping Limited, Charles Nikata, amewataka wafanyabiashara kuitumia bandari hiyo kwa kuwa kwa sasa imeongeza ufanisi wa utendaji kazi wake.

“Tunaishukuru bandari hususan kwa kipindi hiki ambacho imesaidia meli hii kubwa kushusha mzigo wake mapema. Iliingia juzi jioni lakini leo inashusha mizigo, ukiangalia muda uliotumika ni mdogo. Nashauri wafanyabiashara wengine waache kutumia bandari za mbali waje watumie bandari hii,” amesema Nikata.

Naye Captain wa Mv. Mirembe Judith, Cleophas Mufungo, amesema amefurahishwa na utendaji wa bandari hiyo kwa kuwa tangu walivyotia nanga hawakuchukua muda mrefu kushusha mizigo yao.

Mv. Mirembe Judith, ilioyoanza safari zake mwanzoni mwa 2022, sasa inatarajia kupanua wigo wa utoaji huduma katika nchi jirani, ambapo kampuni inayoimiliki, PMM Shipping Limited, inatarajia kuongeza meli nyingine mbili za mizigo na mafuta, ili kutoa huduma bora na nafuu kwa wafanyabiashara hususan wa ndani.

3 Comments

  • Kila la kheir MV Mirembe ,kila la kheir Dr Judith umeupiga mwingi ,daima mbele nyuma mwiko
    PMM INAONGOZA NYENGINE ZINAFUTA.

  • Kwanza mjiulize Sana kwanini watu Wanaona wakatafute Amani waende Mombasa kuliko dar? Shida sio umbali kama ni Amani ktk biashara, dar mmejaa Sana urasimu, kukwamishana, mmekua wakubwa kuliko Mungu mnataka mtukuzwe ndio Tupate Mzigo, usiejulikana au ukiwa huna pesa za hongo huna thamani, watu wamehama mnakuja na meli kubwa hata mje na gumeli gukuuubwaaa KWA adha iliopo afadhali huko mbali…

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Biashara

Sloti ya Mega Jade kasino njia 10 za malipo unaposhinda

Spread the love  TUNAKULETEA mchezo wa kasino wa kufurahisha sana ambapo unapewa...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Biashara

Orb of Destiny kutoka Meridianbet kasino ushindi kwa njia 14  

Spread the love  ORB of Destiny ni mchezo wa sloti kutoka kwa...

error: Content is protected !!