Monday , 13 May 2024
Home Kitengo Biashara Wafanyabiashara Kariakoo waiangukia Serikali
Biashara

Wafanyabiashara Kariakoo waiangukia Serikali

Spread the love

WAFANYABIASHARA waliopoteza mali zao katika ajali ya moto iliyotokea kwenye Soko la Kariakoo, maeneo ya Mnadani, wameiomba Serikali iwasaidie ili waweze kupata mitaji. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Ombi hilo limewasilishwa leo tarehe 2 Oktoba 2023 na Mwenyekiti wa Wafanyabiashara wa Kariakoo, Martin Mbwana, kwa niaba yao wakati wanafanya zoezi la kuokoa mali zilizonusurika kuungua katika ajali iliyotokea asubuhi ya jana Jumapili.

Mbwana alidai kuwa, ajali hiyo  imewaachia msiba wafanyabiashara zaidi ya 1,500 ambao vibanda vyao pamoja na mali vimetekekea kwa moto.

“Kuna wafanyabiashara zaidi ya 1,500 ambao ghafla bin vuu wamekosa biashara, wito wangu kwa Serikali kuja kukaa nao tuwape pole na kuona namna gani wanawasaidia. Huu ni msiba mkubwa moto umeharibu biashara zao zote,” amesema Mbwana.

Katika hatua nyingine, Mbwana ameiomba Serikali iunde timu kwa ajili ya kuchunguza chanzo cha moto ili kibainike kwa ajili ya kuchukua hatua za kudhibiti matukio ya moto kwenye soko hilo.

“Inabidi tuweze kujua moto huu chanzo chake na tukomeshe maana sasa imeshakuwa mazoea Kariakoo moto unatokea ndani ya mwaka mmoja mara tatu. Hii inaathiri mitaji ya watu sisi tunataka tushirikiane nao tukomeshe maana imeshakuwa mazoea,” amesema Mbwana.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Biashara

Meridianbet yatoa msaada Kigamboni siku ya Mama Duniani

Spread the loveMABIBGWA wa michezo ya kubashiri kampuni yaMeridianbet imefika kigamboni leo siku...

BiasharaHabari Mchanganyiko

PPAA yajipanga kuwanoa wazabuni namna kuwasilisha rufaa kieletroniki

Spread the loveIli kukabiliana na mageuzi yaliyofanyika katika Sheria mpya ya Ununuzi...

Biashara

Meridianbet kasino yaja na promo ya mil 200/=

Spread the love  Kimbunga Hidaya kilikuja na madhara makubwa sana katika maeneo...

Biashara

Moon of Thoth, historia ya Misri ya kale ilipofichwa ndani ya kasino

Spread the love  Nchi ya Misri imebeba karibia asilimia kubwa ya mambo...

error: Content is protected !!