Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko WADAU: Ukatili wa kijinsia kazini, unaathiri hadi familia
Habari Mchanganyiko

WADAU: Ukatili wa kijinsia kazini, unaathiri hadi familia

Spread the love

 

WADAU wa ukatili wa jinsia nchini Tanzania, wameshauri waajiri wote pamoja na Serikali kuchukua hatua madhubuti ya kukomesha vitendo vya ukatili vinavyorejesha nyuma maendeleo ya wananchi na jamii kwa ujumla. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Hayo wameyasema leo Ijumaa, tarehe 3 Desemba 2021, jijini Dar es Salaam, katika warsha iliyoandaliwa na Shirika la wanawake katika sheria maendeleo barani Africa (WiLDAF) na kuwakutanisha wadau mbalimbali wakiwemo wabunge, vyama vya wafanyakazi pamoja na Shirika la Kazi Dunia (ILO).

Warsha hiyo inafanyika katika kipindi cha Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia duniani.

Akizungumza katika warsha hiyo, Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Neema Lugangira amesema, suala la ukatili wa jinsia unapaswa kupingwa na makundi ya aina zote na maeneo yote.

“Tunapoongelea ukatili wa kijinsia kazini, tusiwasahau dada wetu wa kazi. Hawa ni watu muhimu zaidi kwani tunapokuwa kwenye shughuli zetu, hawa wanabaki na watoto wetu, tujiulize tunapowalipa Sh.30,000 zinamtosha, huu nao ni moja ya ukatili,” amesema

Amesema, wao kama wabunge, wameendesha kampeni ya kupinga ukatili wa kijinsia mitandaoni kwani “huko nako kunawafanya wanawake, waogope kuingia kwenye siasa, mtu anashambuliwa. Wakiona mimi nashambuliwa, wao wataogopa. Hivyo tusimame kuupinga.”

Aidha, Neema amesema, waajiri wanapaswa kujiuliza katika maeneo ya kazi kuna “chumba cha kunyonyesha watoto, tuangalie hili lipo na kama halipo huu ni ukatili wa kijinsia. Sisi pale bungeni kuna chumba, hivyo wengine waige mfano huu.”

Neema aliungwa mkono na mbunge mwenzake wa viti maalum, Salome Makamba aliyeanza kwa kusema “mimi ni mwathirika namba moja wa ukatili wa kijinsia, mimi ni miongoni mwa wabunge wale COVID-19 kama mnavyosikia, lakini tunapambana.”

Wabunge hao 19 anaowazungumzia ni wale waliokuwa Chadema akiwemo Halima Mdee, waliofukuzwa ndani ya chama chao, lakini bado wapo bungeni.

Salome ametoa wito kwa wadau mbalimbali “kusimama kwa pamoja kupinga ukatili. Unajua ukatili unaumiza, unarudisha nyuma maendeleo katika jamii. Mtu anayefanya ukatili, ajiulize hicho anachokifanya ni sahihi?”

Kwa upande wake, Ofisa Ufuatiliaji na Tathimini wa Wildaf, Rehema Maro alisema katika kipindi cha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia, “ukatili unatokea maeneo ya kazi, hauathiri ofisini tu, unakwenda hadi kwenye ngazi ya familia.”

“Waajiri wanapaswa kujua, ukatili wa kijinsia unawaathiri hadi wao wenyewe kwani aliyefanyiwa hawezi kufanya kazi kwa ufanisi. Hata hata uzalishaji utapungua na hili suala si la kuwaachia vyama vya wafanyakazi, tuungane kwa pamoja,” alisema Rehema

Ameongeza “maeneo ya kazi yawe salama kwa wanawake, watoto na vijana.”

Naye Dk. Katanta Simwanza, ambaye ni mtaalamu wa Saikolojia amesema, “sehemu za kazi ni sehemu ambazo zinapaswa kuwa rafiki, sehemu ya masomo nayo yanapaswa kuwa rafiki kwani inapokuwa si rafiki, molari inaondoka, hivyo tukemee.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Shahidi aeleza namna Nathwani alivyomjeruhi jirani yake

Spread the loveMSIMAMIZI wa Msikiti wa Wahindi Lohana aitwae, Ankit Dawda (32)...

Habari MchanganyikoTangulizi

Kimbunga “HIDAYA” chaendelea kuimarika, wananchi wapewa tahadhari

Spread the loveMAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inaendelea kutoa taarifa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

error: Content is protected !!