Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Ushirikiano: Msimamo mpya wa Lissu
Habari za Siasa

Ushirikiano: Msimamo mpya wa Lissu

Spread the love

TUNDU Lissu, mgombea urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), amesema palipo na mgombea wa Chama cha ACT-Wazalendo, wafuasi wa Chadema wamchague. Anaripoti Mwandishi Wetu, Pemba … (endelea).

Na kwamba, palipo na mgombea wa Chadema, wafuasi wa Chama cha ACT-Wazalendo wamchague, na palipo na wagombea wote, wananchi wapime aliye na nguvu ili kudhibiti mgawnayo wa kura na kutakipa nafasi ya ushindi Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Amesema, msimamo huo unatokana na hatua ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) kuwatema baadhi ya wagombea wa vyama hivyo kutokana na sababu mbalimbali.

Wito huo umetolewa Pemba leo tarehe 22 Oktoba 2020, wakati akizungumza kwenye mkutano wa Maalim Seif Shariff Hamad, mgombea urais wa Zanzibar kupitia ACT-Wazalendo.

“Sasa nyie watu wa Zanzibar ni watu wenye busara,  tusaidieni kutatua hili, mahali ambapo mgombea anayeweza kushinda ni ACT wote twende kwake, na mahali ambako mgombea wa Chadema ana uwezo wa kushinda, wote twende kwake. 

“Adui yetu wa kwanza ni CCM, na mmedhulumiwa muda mrefu, chagueni mbunge ambaye hatahalalisha dhuluma, na hao wagombea wakichaguliwa watafanya kazi na Maalim Seif  kujenga mahusiano mapya kati ya Tanzania na Zanzibar, kusiwe na shaka juu ya wagombea katika hizo nafasi niizosema,” amesema Lissu.

Amesema, uamuzi huo wa kuwaachia wananchi kutumia busara zao kuchagua mgombea mwenye nguvu, unatokana na viongozi wa vyama hivyo kupata muafaka juu ya ushirikiano katika nafasi za ubunge, uwakilishi na udiwani.

“Kuna majimbo ya uwakilishi, kuna wagombea wa ACT-Wazalendo na Chadema majimbo hayo yapo, sasa sisi viongozi kwa bahati mbaya, busara zetu za viongozi hata hapa tulipo tumeshindwa kutatua hili tatizo, nanyi tumsimamishe ndio maana wapo,” amesema Lissu.

Kuhusu maeneo ambayo wagombea wameenguliwa, Lissu amewashauri wafuasi wa vyama hivyo, kuchagua chama ambacho mgombea wake hajaenguliwa.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

error: Content is protected !!