TAREHE 22 Oktoba 1943, ndio siku aliyozaliwa Maalim Seif Sharif Hamad, mgombea urais visiwani Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Pemba … (endelea).
Kwa muktadha huo, Maalim Seif ambaye leo yupo viwanja vya Tibirinzi, Pemba kufunga kampeni zake Pemba. Maalim Seif ametimiza miaka 77.
Maalim Seif aliitwa jukwaani na Salim Biman, Mwenyekiti wa Kamati ya Itikadi, Mawasiliano na Uenezi wa chama hicho.
Kabla ya kupanda jukwaani, Biman alisema “leo kuna tukio kubwa hapa, Maalim Seif alizaliwa tarehe ya leo 22 Oktoba mwaka 1943.”
Baada ya Biman kutoa kauli hiyo, zilisikika kelele za nderemo kuashiria kumpongeza Maalim Seif kwa kuazimisha siku yake ya kuzaliwa.
Hata hivyo, Biman alimwita Maalim Seif jukwaan, naye Maalim Seif alielekea jukwaa huku akisindikizwa na wimbo wa ‘Happy Birthday to You.’
Wakati akieleka jukwaani, keki iliyokuwa imebebwa na mwana mama ambaye amevalia mavazi ya rangi za bendera za chama hicho, aliipeleka jukwaani.
Baada ya hapo, Tundu Lissu ambaye ni mgombea urais wa Tanzania kupitia Chadema, alimfuata Maalim Seif jukwaani na kuanza kucheza wimbo wa ‘Happy Birthday to You’ huku wakishikana mikono.
Sherehe za ‘Happy Birthday to You’ ziliendelea kwa zaidi ya dakika saba jukwaani huku Lissu akimpongeza Maalim Seif pongeze ambazo ziliendana na kicheko.
Tukio hilo limechukua nafasi muda mfupi baada ya Sheikh Ponda Issa Ponda, Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam Tanzania kuwalisha kiapo wafuasi waliohudhuria mkutano huo cha kuwachagua Lissu na Maalim Seif.
Leave a comment