Sunday , 2 April 2023
Home Gazeti Habari za Siasa JPM aeleza alivyoteswa na Mbowe
Habari za SiasaTangulizi

JPM aeleza alivyoteswa na Mbowe

Mgombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya CCM, John Magufuli akihutubia mkutano wa kampeni Shinyanga
Spread the love

MGOMBEA urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli, ameeleza namna Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe alivyomtesa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Kilimanjaro … (endelea).

Akizungumza na wananchi waliohudhuria mkutano wake leo tarehe 22 Oktoba 2020, katika Uwanja wa Half London Boma, Ng’ombe, Hai amesema wananchi hao walimbebesha mzigo kwa kumchagua mbunge wa chama kingine.

Napenda niwaambie wana Hai, kwa kuchagua mbunge kutoka chama kingine, mlinipa kazi kubwa. Mlinibebesha mimi mzigo mkubwa, mlinipa kazi ngumu ya kufanya, kazi ya kuwatumikia. Mlinipa mtihani mkubwa.

“Ilikuwa sawa na kumfunga mtu miguu na mikono yake yote halafu unamwambia nenda kaniletee maji. Nimefungwa miguu, nimefungwa mikono halafu unamwambia, nenda katuchotee maji. Kwangu mimi ilikuwa adhabu,” amesema Dk. Magufuli.

Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema

Akieleza machungu aliyopitia, Dk. Magufuli alikumbushia uongozi wa Mbowe na mgombea ubunge wa jimbo hilo, walivyomgomea katika hotuba yake ya kwanza ya Bunge.

“Wakati naenda kufungua Bunge kwenye hotuba yangu ya kwanza, mwaka 2015 mliviona vitimbwi nilivyofanyiziwa. Haikuishia hapa , kila wakati zilipokuwa zikihitajika fedha kwa ajili ya bajeti, mbunge wenu wa Hai (Mbowe) na wengine wa upinzani walikuwa wanatoka nje.

“Sasa jiulize, tunahitaji barabara ya lami, vituo vya afya, dawa, kero za kiina mama, yule ambaye ni mwakilishi wenu anapoingia bungeni badala ya kuasema hayo, anatoka nje. Ndio maana nasema, nilipata shida sana kuwahudumia wana Hai kwa sababu hapakuwa na connection (muunganiko),” amesema.

Amewaeleza wakazi hao kwamba, yeye ana urafiki na Mbowe ambaye ni Mwenyekiti wa Chadema Taifa, lakini katika hili (la kutoka nje), haungani naye.

 “Mbowe ni rafiki yangu, ninampenda sana, lakini kwenye hili siungani naye. Mimi nimekuwa mbunge kwa miaka 20 kwenye jimbo langu, unapokuwa mbunge, kazi moja ya mbunge ni kujenga mahusiano na mawaziri,” amesema.

 Amesema, miaka mitano iliyopita alifika kwenye jimbo hilo kuomba kura pia kumwombea mbunge na wadiwani wa jimbo hilo, hata hivyo walichagua madiwani wachache wa CCM na  hawakuchagua mgombea aliyetokana na chama hicho.

“Miaka mitano iliyopita tulipokuja kuomba kura, nikamuombea mbunge wa CCM, nikawaombea pia madiwani wa CCM, nashukuru sana wana Hai mlinichagua kuwa rais wenu, hata hivyo kwa nafasi ya ubunge mlimchagua mtu kutoka chama kingine, na pia mlichagua madiwani wengi kutoka chama kingine,” amesema.

Dk. Magufuli amewaomba wananchi hao kuchagua wagombea wa CCM kwenye jimbo hilo, ili afanye nao kazi ya kupeleka mbele maendeleo ya jimbo na mkoa huo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Samia apangua mawaziri

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan, amefanya mabadiliko madogo ya Baraza la...

Habari za Siasa

RC mstaafu afariki dunia, CCM yamlilia

Spread the loveALIYEWAHI kuwa mkuu wa mikoa ya Dodoma, Mara, Mtwara na...

Habari za Siasa

Marekani kuwekeza Dola 500 Mil kupeleka bidhaa na huduma Tanzania

Spread the loveMAKAMU wa Rais wa Marekani, Kamala Harris amesema miongoni mwa...

Habari za Siasa

Kamala ataja hatua mpya kuimarisha uhusiano wa kibiashara Tanzania, Marekani

Spread the loveKATIKA kuimaridha uhusiano wa kibiashara na kiuchumi baina ya Tanzania...

error: Content is protected !!