February 25, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Upinzani wazidi kupukutika, Meya Ilala abwaga manyanga

Spread the love

OMARY Kumbilamoto, Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala, ambaye pia ni Diwani wa kata ya Vingunguti kupitia tiketi ya Chama cha Wananchi CUF, leo tarehe 1 Agosti, mwaka huu, ametangaza kujiudhuru uanachama wa chama chake na nafasi zote alizokuwa nazo. Anaripoti Faki Sosi … (endelea)

Kumbilamoto amesema kuwa amechukua uamuzi huyo kutokana na vitisho anavyopewa na viongozi wa chama hicho pindi amepoungana na viongozi wa serikali katika kutekeleza majukumu ya kuwatumikia wananchi.

“Nimejivua uanachama wa CUF na nafasi zangu zote ndani ya chama ikiwemo ya udiwani katika kata ya Vingunguti pia unaibu meya wa manispaa na nimechukua hatua ili kulinda na kutetea maslahi ya wananchi ninaowatumia hivyo ili niendelee kuteleza majukumu yangu ipasavyo najivua ili kuunga mkono jitihada za rais Magufuli na viongozi wote Serikali kwa ujumla,” amsema Kumbilamoto.

Ameongeza kuwa ndani ya chama cha wananchi Cuf kuna mgogoro ambapo ameufananisha na mgogoro wa nchi za Israel na Palestina, kwani hauna suluhu, hivyo mara nyingi nimekuwa nijikita zaidi kusaidia kutatua changamoto za wananchi lakini viongozi wananitishia kunivua uanachama hivyo ni maamuzi magumu niliyoyafanya kwa wananchi wangu ila imenilazimu kufanya hivyo ili niwe huru kwa sasa.

Ameongeza kuwa katika miaka miwili ya udiwani ametekeleza ahadi mbalimbali ikiwemo kununua Ambulance ya wagonjwa kukarabati hospitali, lakini cha kushangaza kipindi cha masika wananchi walipata madha lakini hajawahi kuona kiongozi yeyote wa chama cha CUF akienda kusaidia au kuzungumza chochote zaidi ya Mkuu wa Mkoa na Wilaya ambao walikwenda kuona na kuwasaidia.

error: Content is protected !!