March 8, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Uwanja wa ndege mpya wakamilika asilimia 8o

Spread the love

MHANDISI Isack Kamwelwe, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, amefanya ziara katika kiwanja kipya cha ndege cha Julius Nyerere kilichopo DSM kufanya ukaguzi wa ujenzi wa kiwanja hicho. Anaripoti Khalifa Abdallah … (endelea).

Mhandisi Kamwelwe amefanya ziara hiyo ikiwa ni siku yake ya 19 tangu kuteuliwa kuwa Waziri mwenye dhamana na ujenzi, ambapo kiwanja hicho kinatarajiwa kukamilika Mei, 2019. 

Akizungumza na waandishi wa habari, Waziri Kamwelwe amesema kuwa serikali imeridhika na hali ya ujenzi huo ambapo hadi sasa umefikia zaidi ya asiilimia 78 na kiwanja hicho kinatarajiwa kuchukua abiria Milioni 6 kwa mwaka.

“Terminal 1 imejengwa mwaka 1956 na ilikuwa na uwezo wa kupokea abiria laki 5 kwa mwaka Terminal 2 imejengwa mwaka 1984 ilikuwa na uwezo wa kupokea watu milioni 1.5 kwa mwaka, lakini sasa hivi Terminal 2 inakwenda mpaka watu Milioni 2.5 kwa mwaka lakini Serikali ikaona kuna umuhimu wa wa kuongeza Terminal nyingine ya tatu ambayo itapokea watu Milioni 6,” amesema.

Kamwelwe amesema kwa mujibu wa wataalamu huduma hiyo ambayo imewekezwa inaweza kufika hadi mwaka 2035 ambapo uwanja huo utakuwa na uwezo wa kupaki ndege kubwa 13 kwa wakati mmoja.

Katika hatua nyingine Kamwelwe amemuagiza Mhandisi Mshauri wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini (TAA) ndani ya siku 7 kuripoti TANROADS akiwa na nyaraka zake ili zikafanyiwe kazi na TANROADS.

“Rais ametoa Instrument ya kujenga viwanja vya ndege katika taifa letu na Instrument hiyo wamepewa TANROADS kwa hiyo shughuli zote za ujenzi wa viwanja zitafanywa na TANROADS,” amesema.

error: Content is protected !!