February 24, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mkwasa kwenda India kwa Matibabu

Boniface Mkwasa

Spread the love

ALIYEKUWA katibu mkuu wa klabu ya Yanga na kocha wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) Charles Boniface Mkwasa amesafiri jana kuelekea India kwa matibabu ya maradhi yanayomkabili. Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea).

Taarifa hiyo ya matibabu ya Mkwasa imetolewa na Msemaji wa klabu hiyo Dismas Ten kupitia ukurasa wake unaopatikana kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram uliosomeka.

“Kila la kheri Mkwasa kwenye safari yako ya matibabu India, imani yangu kubwa kila kitu kitakwenda sawa na utarejea kwenye afya yako”

Mkwasa ambaye alijiuzuru kwenye nafasi yake ya ukatibu mkuu ndani ya klabu ya Yanga mapema mwezi uliopita kutokana na sababu za maradhi ambayo yanamkabili kwa sasa.

error: Content is protected !!