December 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Upelelezi wakwamisha kesi ya Wema

Wema Sepetu (kulia) akitoka na mama yake mahakamani Kisutu

Spread the love

KESI ya kuchapisha na kusambaza video ya ngono inayomkabili msanii wa filamu nchini, Wema Sepetu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeahirishwa hadi tarehe 12 Desemba 2018, kutokana na upande wa mashtaka kutokamilisha upelelezi. Anaripoti mwandishi Wetu … (endelea).

Kesi hiyo iliyofunguliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) dhidi ya Wema, leo tarehe 21 Novemba 2018 ilitakiwa kutajwa tarehe, lakini imeahirishwa kutokana na upande wa mashtaka kutokamilisha upelelezi wa kesi hiyo.

Hakimu anayesimamia kesi hiyo, Hakimu Maira Kasonde aliiahirisha kesi hiyo. Upande wa jamhuri unasimamiwa na Wakili Jenifer Masue huku wakili wa utetezi akiwa Ruben Simwanza.

Mnamo tarehe mosi Novemba 2018 Wema alipandishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, ikiwa siku kadhaa zimepita tangu aliposambaza mitandaoni video yake inayomuonyesha akiwa faragha na mpenzi wake anayefahamika kwa jina la PCK.

error: Content is protected !!