Spread the love

 

WAZIRI wa Afya, Ummy Mwalimu amekutana na viongozi wa idara ya kinga na kufanya mapitio ya pamoja kuhusu mafanikio, changamoto na vipaumbele katika kuimarisha huduma za kinga ili kupunguza maradhi, ulemavu. Anaripoti Danson Kaijage – Dodoma …(endelea)

Kikao hicho kimefanyika jana tarehe 17 Januari, 2022 katika ofisi za Wizara ya Afya jijini Dodoma na kuhudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof. Abel Makubi pamoja na Mganga Mkuu wa Serikali Dk. Aifello Sichalwe.

Katika kikao hicho, Ummy amesisitiza juu ya kuboresha utoaji huduma kwa wananchi ili kupunguza kero na malalamiko katika jamii ikiwemo huduma za lishe pamoja na mama na mtoto.

Mapitio yaliyofanywa kwenye kikao ni pamoja na ufuatiliaji na udhibiti wa magonjwa, huduma za chanjo, afya ya uzazi na mtoto, huduma za lishe, afya mazingira, elimu ya afya kwa umma.

Aidha, wamejadili mikakati mbalimbali ya mapambano dhidi ya UVIKO-19, magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele(NTDs), malaria, kifua kikuu, ukoma na Ukimwi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *