Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Uchaguzi ubunge Konde, Ushetu Oktoba 9
Habari za SiasaTangulizi

Uchaguzi ubunge Konde, Ushetu Oktoba 9

Mkurugenzi wa Uchaguzi, Dk. Wilson Mahera
Spread the love

 

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imetangaza uchaguzi wa marudio wa ubunge katika majimbo ya Konde mkoa wa Kaskazini Pemba na Ushetu mkoani Shinyanga utafanyika tarehe 9 Oktoba 2021. Anaripoti Victoria Mwakisimba, TUDARCo … (endelea).

Ni baada ya majimbo hayo kuwa wazi, kutokana na vifo vya Elias Kwandikwa wa Ushetu (CCM), aliyekuwa waziri wa ulinzi na jeshi la kujenga Taifa pamoja na Khatibu Said Haji wa Konde kupitia ACT-Wazalendo.

Haji alifariki dunia tarehe 20 Mei 2021, katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam na uchaguzi wa marudio ulifanyika tarehe 18 Julai 2021 na Sheha Mpemba Faki wa CCM, aliibuka mshindi.

Hata hivyo, tarehe 2 Agosti 2021, Faki alitangaza kujiuzulu akitoa sababu za zilizomfanya kujiweka kando ni za kifamilia.

Naye Kwandikwa alifariki dunia tarehe 3 Agosti 2021, katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alipokuwa akipatiwa matibabu.

Elias Kwandikwa

Leo Ijumaa, tarehe 27 Agosti 2021,  Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Dk. Wilson Mahera amesema, ratiba ya uchaguzi huo ipo tayari.

Dk. Mahera amesema, NEC imepokea barua kutoka kwa Spika wa Bunge la Tanzania yenye Kumb. Na. CEA.137/400/02/111 ya tarehe 16 Agosti 2021, akiitaarifu kuhusu kuwepo kwa nafasi wazi ya Ubunge Jimbo la Ushetu mkoani Shinyanga.

Nafasi hiyo inatokana na kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo, Elias John Kwandikwa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Dk. Mahera amesema taarifa hiyo ya Spika ni kwa mujibu wa kifungu cha 37(3) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343.

Aidha, kwa upande wa Jimbo la Konde, Dk Mahera amesema mnamo tarehe 2 Agosti, 2021 Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilitoa taarifa kwa umma kuhusu kuwepo wazi kwa  Jimbo la Konde lilipo katika Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba kutokana  na mbunge mteule wa jimbo hilo,  Sheha Mpemba Faki kujiuzulu.

Sheha Mpemba Faki

Amesema, tume ilipokea barua yenye Kumb. Na. CMM/T.40/Vol.I/72 ya tarehe 2 Agosti, 2021 kutoka kwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ikitoa taarifa kuwa Mbunge Mteule wa Jimbo la Konde, ameandika barua, kueleza hakuwa tayari kuwawakilisha wananchi wa Konde kutokana na changamoto za kifamilia.

Dk. Mahera amesema, kutokana na hatua hiyo, Tume ililitangaza jimbo hilo kuwa wazi kwa kuwa Mbunge huyo Mteule alikuwa bado hajatangazwa katika Gazeti la Serikali kwa mujibu wa kifungu cha 81(c) (iii) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343.

Maandalizi kwa ajili ya uchaguzi huo yameshafanyika na kazi ya utoaji fomu za uchaguzi kwa wagombea inaanza tarehe 13-19  Septemba 2021 huku uteuzi wa wagombea watakao wania nafasi hizo ukifanyika  19 Septemba 2021.

Aidha, Dkt Mahera amesema kampeni za uchaguzi katika majimbo hayo ya Ushetu na Konde utaanza 20 Septemba  2021 na zitafikia ukomo wake 8 Oktoba na uchaguzi kufanyika 9 Oktoba 2021.

Dk Mahera amesema, Tume ya Taifa ya Uchaguzi inavikumbusha vyama vya siasa na wadau wote wa uchaguzi kuzingatia sheria, kanuni, maadili ya uchaguzi, taratibu, miongozo na maelekezo yatakayotole wa na Tume katika kipindi cha Uchaguzi mdogo.

1 Comment

  • Wewe mahera mpumbavu tunashangaa kuwa bado tu umekikalia kiti utazani umegandishwa na gundi au hadi tufanyiane kitu mbaya kama alichokifanya hamza ndio msome alama za nyakati?.Waaminishe hao hao wajinga wenzako kwamba faki Mpemba kajiuzulu ubunge kwa sababu za ki familia,kwa watu kama sisi wenye kujuwa na kuona,hakuna kitu kama hicho mlipora uchindi wa chama cha ACT mchana kweupe dunia mzima ilishuhudia na chama mlicho kipora kilikusudia kiishangaze dunia kwa maamuzi waliyotaka kuyachukua na ndio sababu rais samia na dk hussein wakaingolia kati,rai yangu mkubali makosa mkubali mlipo jikwaa na kuingia tena katika uchaguzi 20/Septemba.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

error: Content is protected !!