May 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Nandy, Koffie kupagawisha wanayanga Jumapili

Spread the love

NGULI wa muziki barani Afrika kutoka Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, Koffie Olomide pamoja na msanii mashuhuri kutoka nchini Tanzania Nandy wanatarajia kutoa burudani kwenye kilelel cha Tamasha la siku ya Mwananchi. Anaripoti Mintanga Hunda, TUDARCo…(endelea)

Tamasha hilo litafanyika Agosti 29, kuanzia Asubuhi kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam.

Kuelekea kilelel cha tamasha hilo msanii wa kizazi kipya Nandy, siku ya jana aliachia wimbo maalumu, ambao unafahamika kwa jina la Yanga ambao pia atautumbuiza kwenye Tamasha hilo.

Moja ya shughuli ambazo zitafanyika kwenye tamasha hilo ni pamoja na kutambulisha wachezaji wapya pamoja na waliokuwepo kuelekea msimu mpya wa mashindao, sambamba na benchi la ufundi.

Yanga wanakwenda kwenye tukio hilo huku tayari wakiwa wameshatambulisha jezi zao mpya za nyumbani na ugenini siku ya Jumatano Agosti 25, mwaka huu kwenye ukumbi wa Mlimani City.

Kwa upande wa Koffie amethibitisha rasmi kuwepo kwenye siku hiyo ambayo pia Yanga itacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Zanaco kutoka Zambia.

error: Content is protected !!