Wednesday , 8 February 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko RC Makalla: Majeruhi tukio la mauaji Dar wanaendelea vizuri
Habari Mchanganyiko

RC Makalla: Majeruhi tukio la mauaji Dar wanaendelea vizuri

Amos Makala, Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam
Spread the love

 

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam (RC) nchini Tanzania, Amos Makalla, amesema majeruhi wa tukio la mauaji lililotokea jirani na Ubalozi wa Ufaransa nchini humo, wanaendelea vizuri. Anaripoti Mwanaharusi Abdallah, TUDARCo … (endelea).

Makalla ametoa taarifa hiyo leo Ijumaa, tarehe 27 Agosti 2021 katika shughuli ya kuiaga miili ya Askari Polisi watatu na mlinzi mmoja wa Kampuni ya Ulinzi ya SGA, iliyofanyika viwanja vya Polisi, Kurasini mkoani Dar es Salaam.

Amesema jana Alhamisi alitembelea Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na Hospitali ya Polisi Kilwa Road Kurasini, na kuzungumza na majeruhi hao.

“Jana mimi na wenzangu tulikuja hospitali mochwari tuliwaona wote pamoja na mhalifu, vijana wadogo ambao walikuwa tegemeo kwa nchi yetu.”

“Hatukuishia hapo, tulikwenda kuwaona majeruhi wote mmoja wa hapa na mwingine Muhimbili, niseme watapona tumewaona wameeleza kwa kina tukio lilivyotokea itoshe kusema tumepoteza mashujaa,” amesema Makalla.

Pia, mkuu huyo wa mkoa ametoa rambirambi ya Sh.6 milioni na kumpatia Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Simon Sirro atakayezigawa kwa familia za marehemu wote wanne.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mawakili waiburuza mahakamani TLS, EALS

Spread the love  WAKILI Hekima Mwasipu na wenzake wawili, wamefungua kesi katika...

Habari Mchanganyiko

Uvuvi bahari kuu wapaisha pato la Taifa

Spread the love  SERIKALI imesema uvuvi wa bahari kuu umeliingizia Taifa pato...

Habari Mchanganyiko

DPP aweka pingamizi kesi ya ‘watu wasiojulikana’

Spread the love  MKURUGENZI wa Mashtaka nchini (DPP), ameweka pingamizi dhidi ya...

Habari Mchanganyiko

Washindi saba safarini Dubai NMB MastaBata ‘Kote Kote’

Spread the loveKAMPENI ya kuhamasisha matumizi ya Mastercard na QR Code ‘Lipa...

error: Content is protected !!