Monday , 11 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Ubunge Viti maalum: Wajumbe UVCCM kazini leo
Habari za SiasaTangulizi

Ubunge Viti maalum: Wajumbe UVCCM kazini leo

Mkutano Mkuu wa CCM
Spread the love

WAJUMBE wa Mabaraza ya Vijana ya Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) wa mikoa nchini Tanzania, leo Alhamisi tarehe 30 Julai 2020, watapiga kura za maoni za ubunge wa viti maalum katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Kwa mujibu wa ratiba ya mchakato wa kuwapata wagombea wa CCM katika nafasi za ubunge, uwakilishi na udiwani kwenye uchaguzi huo, Baraza la Vijana la Mkoa linapiga kura hizo ili kupeleka mapendekezo yake kwa Baraza Kuu la Jumuiya ya Vijana (UVCCM).

Baada ya wajumbe wa Baraza la Vijana Mkoa kuwasilisha mapendekezo yake katika Baraza Kuu la UVCCM, tarehe 8 Agosti 2020, baraza kuu hilo litapiga kura za maoni kwa wagombea wa ubunge na uwakilishi viti maalum kundi la vijana.

Kura za maoni CCM kupendekeza wabunge na wawakilishi viti maalum kundi la vijana, zitafuatiwa na kura za maoni kwa wagombea viti maalum kundi la wazazi, zitakazofanyika kesho Ijumaa tarehe 31 Julai 2020.

Baraza la Wazazi Mkoa litafanya kura za maoni, kisha tarehe 9 Agosti 2020, Baraza Kuu la Wazazi litapiga kura za maoni kwa wagombea ubunge na uwakilishi viti maalum kundi la wazazi.

CCM ilifungua zoezi la kutafuta wagombea wake katika uchaguzi huo tarehe 14 Julai 2020, ambapo watia nia katika nafasi mbalimbali walianza kuchukua siku hiyo, na kisha kurejesha fomu hizo tarehe 17 Julai 2020.

Hadi sasa, CCM imeshapitisha wagombea Urais wa Tanzania na Zanzibar, ambapo Rais John Magufuli alipitishwa na Mkutano Mkuu wa chama hicho kugombea Urais wa Tanzania huku Dk. Hussein Ali Mwinyi akipitishwa kuwa Mgombea Urais wa Zanzibar.

Hali kadhalika, CCM imeshakamilisha kura za maoni kwa wagombea ubunge na uwakilishi wa majimbo pamoja na kura za maoni za wabunge wa viti maalum kwa wagombea viti vya Mkoa na makundi mengine isipokuwa ya vijana na wazazi.

Pia, leo Alhamisi tarehe 30 Julai 2020, vikao vya kamati za siasa jimbo vinakutana kwa siku moja kuwajadili wagombea ubunge na kutoa mapendekezo yake kwa kamati za siasa za wilaya.

Shughuli kama hiyo, itafanyika kwa kamati ya siasa Jimbo kuwajadiuli wagombea Uwakilishi upande wa Zanzibar na kutoa mapendekezo kamati za siasa za wilaya.

Kheri James, Mwenyekiti wa UVCCM

Jana Jumatano tarehe 29 Julai 2020, vikao vya kamati za siasa za CCM Kata Tanzania Bara na Wazi upande wa Zanzibar zilikutana kuwajadili wagombea na kutoa mapendekezo yake kwa kamati za siasa za Jimbo (Zanzibar) na Wilaya (Tanzania bara).

Leo Alhamisi, vikao vya kamati za siasa za CCM jimbo Zanzibar, kuwajadili wagombea na kutoa mapendekezo yake kwa kamati za siasa za wilaya.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Jaji Kiongozi akerwa wananchi kukosa imani na mahakama

Spread the loveWATENDAJI wa Mahakama ya Tanzania, wametakiwa kuweka mikakati itakayosaidia kurejesha...

BurudikaHabari za Siasa

Samia amchangia Professa Jay mil. 50, Chadema, wasanii wamwaga manoti

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan amechangia kiasi cha Sh 50 milioni...

Habari za Siasa

Biteko: Samia ni muumini wa maridhiano sio kwa kuigiza

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Mpango: Sitakufa bali nitaishi

Spread the loveMAKAMU  wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk....

error: Content is protected !!