Saturday , 22 June 2024
Home Gazeti Tangulizi Mkapa ahitimisha safari ya siku 29,845 duniani
Tangulizi

Mkapa ahitimisha safari ya siku 29,845 duniani

Spread the love

BENJAMIN William Mkapa, Rais mstaafu wa awamu ya tatu wa Tanzania, amehitimisha safari yake ya siku 29,845 hapa duniani. Anaripoti Hamisi Mguta, Lupaso, Masasi … (endelea)

Safari yake imehitimishwa leo Jumatano tarehe 29 Julai 2020 saa 9:03 alasiri wakati jeneza lililobeba mwili wake likishushwa kwenye makazi yake mapya ya milele katika kijiji kilekile alichozaliwa Lupaso, wilayani Masasi Mkoa wa Mtwara.

Marehemu Benjamin Mkapa

Ilipofika saa 9.21 alasiri, Askari wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) walianza kufunika kwa juu kaburi hilo kisha utaratibu mwingine wa jeshi uliendelea ikiwemo upigwaji wa mizinga 21.

         Soma zaidi:-

Vilio na majonzi vilitawala kijijini hapo kwa waombolezaji wakiongozwa na Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli waliposhuhudia jeneza lenye mwili wa Mkapa likishuka taratibu kaburini.

Mama Anna, mjane wa Mkapa alianza kububutikwa machozi, hali iliyowafanya wasaidizi wake mmoja wa watu waliokuwa wakimsaidia kumfuta machozi huku Rais Magufuli aliyekuwa amekaa kushoto kwake, akionekana akimfariji.

Wapo waliokuwa wakifuta machozi kwa kutumia vitambaa vyao, kuhitimisha uwepo wake hapa duniani kwa Mkapa au jeneza lenye mwili wake kutoonekana tena katika uso wa dunia.

Mkapa aliyezaliwa kijijini hapo tarehe 12 Novemba 1938, alifariki dunia Alhamisi iliyopita tarehe 23 Julai 2020 saa 3:30 usiku katika moja ya hospitali jijini Dar es Salaam kwa mshtuko wa moyo.

Kuanzia tarehe 12 Novemba 1938 hadi leo Jumatano tarehe 29 Julai 2020 ni sawa na siku 29,845 ambazo ni miezi 980 na siku 17.

Pia, ni sawa na saa 716,280 na wiki 4,263 alizotumia kuwa katika uso wa dunia.

Mkapa aliongoza Tanzania kwa nafasi ya juu ya uongozi kwa miaka kumi mfululizo kuanzia mwaka 1995 akichukua nafasi iliyokuwa imeachwa na Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi hadi mwaka 2005 alipomwachia kijiti, Jakaya Mrisho Kikwete.

Kikwete aliongoza kwa miaka kumi kati ya mwaka 2005 hadi 20015 alipomwachia Rais John Pombe Magufuli anayeendelea kuongoza mpaka sasa.

Mkapa amehitimisha safari yake akiacha mjane, Mama Anna na watoto wawili wa kiume, Stephano na Nicholas.

Mkapa ameondoka katika uso wa dunia akiwa ameacha kitabu kinachoelezea maisha yake cha My Life, My Purpose (Maisha Yangu, Kusidio Langu) kilichozinduliwa tarehe 12 Novemba 2019 siku aliyotimiza miaka 80.

Kabla ya mazisho kufanyika, yalitanguliwa na misa iliyoongozwa na Rais wa Baraza la Maaskaofu Katoliki Tanzania (TEC), Gervas Nyaisonga kijijini hapo na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiongozwa na Makamu wa Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.

Wengine waliohudhuria misa hiyo ni Marais wastaafu; Ali Hassan Mwinyi na Jakaya Mrisho Kikwete.

Pia, walikuwapo, Rais wa Zanzibar, Ali Mohamed Shein, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi, Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Askofu Wolfang Rais mpya TEC, Padri Kitima aula tena

Spread the loveBARAZA la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) limetambulisha safu mpya za...

Habari MchanganyikoTangulizi

Padre anayetuhumiwa mauaji ya Asimwe, asimamishwa

Spread the loveKanisa Katoliki Jimbo la Bukoba limemsimamisha kutoa huduma za kichungaji...

Habari za SiasaTangulizi

Bashe apasua mtumbwi CCM

Spread the love  HUSSEIN Mohammed Bashe, waziri wa Kilimo, amekiweka pabaya Chama Cha...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Baba mzazi, mganga, paroko wadakwa mauaji ya mtoto mwenye ualbino

Spread the loveHATIMAYE Jeshi la Polisi limewakamata watuhumiwa tisa wakiwa na viungo...

error: Content is protected !!