Friday , 29 September 2023
Home Kitengo Michezo Tunduma watenga billioni 1.5 kujenga uwanja
Michezo

Tunduma watenga billioni 1.5 kujenga uwanja

Spread the love

KUTOKANA na ukosefu wa eneo sahihi la kufanyia michezo halmashauri ya mji Tunduma wilayani Momba mkoani Songwe imetenga kiasi cha Sh.1.5 bilioni kujenga uwanja wa kisasa ili kukuza vipaji vya michezo kwa vijana na kuwa chanzo cha mapato. Anaripoti Ibrahim Yassin, Songwe …(endelea).

Akizungumza ofisini kwake leo tarehe 6 Julai 2023, Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Utamaduni Sanaa na Michezo wa Halmashauri hiyo, Rashid Mwalugi amesema kwa muda mrefu Tunduma hakuna uwanja wa michezo wenye sifa ya kimichezo.

Mwenyekiti wa halmashauri ya mji huo, Ayoub Mlimba

Amesema halmashauri kupitia mapato yake ya ndani imetenga kiasi hicho cha fedha kujenga uwanja eneo la Mpemba utakaotumika kwa michezo yote ikiwemo mpira wa miguu.

Amesema tayari eneo limesawazishwa na kumwaga tofali 15,000 za uzio uchimbaji wa msingi tayari kwa ujenzi na ifikapo mwaka 2024 uwanja utakuwa umekamilika.

Ameongeza kuwa hadi sasa Tunduma ina timu 30 za mpira wa miguu kati ya hizo timu 12 pekee ndizo zilizosajiliwa.

Amesema timu za mpira wa mikono (Netball) zipo 6 kati ya hizo 3 zimesajiliwa pia kuna timu ya Maendeleo Queens inayoshiriki ligi ya daraja la kwanza.

“Ili kuhakikisha mpira wa miguu unakua vipo vituo (academy) mbili zinazosaidia kulea na kukuza vipaji vya watoto zikiwa chini ya Mwalimu Minga (kocha mototo)… tunampa ushirikiano wa karibu,” amesema Mwalugi.

Mwalugi ameongeza kuwa lengo la mradi ni kutanua wigo na kukuza vipaji vya vijana kwenye tasnia zote ikiwemo michezo, kuvutia wawekezaji na mama lishe watakaokuja kuwekeza na kuanzisha biashara zao eneo hilo.

Mwenyekiti wa halmashauri ya mji huo, Ayoub Mlimba amesema kutokana na umuhimu wa michezo kupitia baraza lao la madiwani walipitisha Sh 1.5 bilioni kujenga uwanja huo.

Ayoub Mlimba mwenyekiti wa halmashauri ya mji Tunduma akielezea umuhimu wa uwanja.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Meridianbet yaibukia Tandika, yafungua duka jipya

Spread the love BAADA ya kupita maeneo mbalimbali hatimae kampuni yaMeridianbet imeibukia...

BiasharaMichezo

Ukiwa na Meridianbet ni rahisi kuwa milionea

Spread the love  CARABAO Cup raundi ya 3 Uingereza inaendelea na mechi...

Michezo

Jezi ya Samatta iliyoifunga Liverpool kuuzwa Genk

Spread the love  KLABU ya KRC Genk ya nchini Ubelgiji imeamua kuanza...

BiasharaMichezo

Hii ndio historia ya El-Clasico, derby bora zaidi duniani

Spread the love  KILA nchi ina vilabu viwili hasimu na pinzani nje...

error: Content is protected !!