Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Tangulizi Tundu Lissu atuma salamu NEC
Tangulizi

Tundu Lissu atuma salamu NEC

Spread the love

TUNDU Lissu, mgombea mteule wa urais kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), ametuma salamu kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC). Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea). 

Kupitia ukurasa wake wa Twitter leo Jumanne tarehe 4 Agosti 2020, Lissu ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Chadema Taifa, amesema ni muda wa upinzani kuishinikiza NEC kutenda haki katika mchakato wa uchaguzi huo, hususan katika uteuzi wa wagombea.

 Lissu amesema, upinzani hautakubali jambo lolote isipokuwa uchaguzi huru, haki na wenye ushindani mzuri.

“Sasa ni muda wa kuidai NEC kutowaengua wagombea wetu. Hatutakubali chochote isipokiwa uchaguzi wenye ushindani huru na haki,” amesema Lissu.

Mwenyekiti wa NEC, Semistocles Kaijage

Lissu ametoa ujumbe huo kwa NEC siku moja baada ya wajumbe wa Baraza Kuu la chama hicho  kupendekeza kupelekwa jina lake katika Mkutano Mkuu unaofanyika leo, kuwa mgombea wa urais wa Tanzania Bara.

Katika kura zilizopigwa na Baraza Kuu la chama hicho jana Jumatatu tarehe 3 Agosti 2020, wajumbe wa baraza hilo walimpendekeza Lissu kuwamgombea, akiwashinda Lazaro Nyalandu, Mwenyekiti Chadema Kanda ya Kati na Dk. Mayrose Majinge.

Lissu alishinda kwa kura 405 kati ya kura za wajumbe 442 wa baraza hilo waliopiga kura jana kwenye Ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam.

Wananchi wakiwa katika foleni ya kupiga kura

Nyalandu alishika nafasi ya pili kwa kura 36 na Dk. Mayrose akiambulia kura moja.

Ikiwa Mkutano Mkuu wa leo utampitisha, Lissu anakwenda kuchuana na mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais John Pombe Magufuli ambaye naye amekwisha kupitishwa na chama chake.

Wagombea wengine wa urais na vyama vyao kwenye mabano ni Profesa Ibrahim Lipumba (CUF), Hashimu Rungwe (Chaumma) na John Shibuda wa Ade- Tadea.

Tundu Lissu, Makamu Mwenyekiti wa Chadema

Akizungumzia ushindi wa Lissu, Nyalandu amempongeza mwanasiasa huyo kwa ushindi, huku akimuahidi kumpa ushirikiano katika harakati zake za kugombea  Urais wa Tanzania.

“Pongezi sana kaka Tundu Lissu kwa ushindi wa kishindo ulioupata Baraza Kuu Chadema kuwa mgombea urais kupitia chama chetu. Nakupongeza kwa dhati na tutashirikiana kuhakikisha chama chetu kinashinda Oktoba 28, 2020,” ameandika Nyalandu katika ukurasa wake wa Twitter.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za SiasaTangulizi

Shibuda amlima waraka mzito Bulembo

Spread the loveMKONGWE wa siasa nchini, John Shibuda amemshukia kada maarufu wa...

error: Content is protected !!