September 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Vigogo KDCU kortini tuhuma za utakatishaji milioni 900

Spread the love

WATU 11 wakiwemo viongozi wa Chama Kikuu cha Ushirika wilayani Karagwe (KDCU LTD), Mkoa wa Kagera wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Bukoba kwa kosa la utakatishaji fedha kiasi cha Sh. 900 Milioni. Anaripoti Mwandishi Wetu, Kagera … (endelea).

Watuhumiwa hao 11 wamefikishwa mahakamani hapo jana Jumatatu tarehe 3 Agosti 2020, na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Kagera kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka mkoani humo. 

Taarifa hiyo imetolewa jan Jumatatu na John Joseph, Mkuu wa Takukuru mkoani Kagera.

Sambamba na utakatishaji fedha, watuhumiwa hao wamepandishwa mahakamani hapo kujibu mashtaka ya rushwa na uhujumu uchumi.

Taarifa ya Joseph ilieleza watuhumiwa, hao wamefikishwa mahakamani ili kujibu tuhuma  15 zinazowakabili zikiwemo makosa ya rushwa na jinai ikiwemo matumizi mabaya ya madaraka, kutoa nyaraka za uongo kinyume cha sheria.

“Kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu, kusababisha hasara kinyume na aya ya 10(1) ya jedwali la kwanza ikisomwa pamoja na kifungu cha 57(1) na kifungu cha 60(1) vya sheria ya uhujumu uchumi sura ya 200 toleo la 2002,” inaeleza taarifa ya Joseph.

Afisa Uhusiano wa Takukuru, Doreen Kapwani

Mkuu huyo wa Takukuru alisema, watuhumiwa hao wamefikishwa mahakamani baada ya uchunguzi wa taasisi hiyo kubaini waliingia mkataba mbovu wa ukarabati wa Hoteli ya Coffee Trees inayomilikiwa na KDCU LTD, uliosababishia chama hicho hasara ya Sh. 900 milioni.

“Takukuru ilianzisha uchunguzi kufuatia kupokelewa kwa taarifa mnamo mwaka 2016 na uchunguzi uliofanyika umeweza kubaini mnamo mwaka 2008 uongozi uliokuwa wa KDCU uliingia mkataba wa ukarabati wa hoteli hiyo.”

“Mkataba wa mashaka na kutokana na kuingiwa kwa mkataba huo watuhumiwa kwa nyakati tofauti tofauti kuanzia mwaka 2008 hadi 2011 waliweza kutenda makosa tajwa na kusababisha hasara ya zaidi ya Sh. 900 Mil kwa KDCU,” ilieleza taarifa ya Joseph.

Brigedia Jenerali, John Mbungo, Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru

Watuhumiwa hao ni, Prospery Kashangaki Murungi, Mwenyekiti mstaafu wa Bodi ya  KDCU LTD, Anna Michael Mlay, aliyekuwa  Meneja Utumishi na Utawala KDCU LTD. Sylvery, aliyekuwa Mkaguzi Mkuu wa ndani KDCU LTD na Justin Tinkaligaile Fidelis, Mkazi wa Kata ya Nyakahanga Karagwe.

Wengine ni, Cyril Tambala Protase, Mkazi wa Rwabere –Kyerwa, Adriani Rwechungura Kabushoke, mkazi wa Rugu Karagwe, Sylvester  Joseph Mugishagwe Mkazi wa Dar es Salaam na mfanyakazi wa Kampuni ya DAN CONSTRUCTION  (T) LTD.

Pia wamo, watumishi wawili wastaafu wa Ofisi ya Katibu Tawala mkoani Kagera, Nestory Tiibaza na Emanuel Ndyamukama.

Josephati Kinyina, mkazi wa Nyabiyonza Karagwe na Desderius Rutakyamirwa  Mkazi wa Dar es Salaam na mfanyakazi wa Kampuni ya DAN CONSTRUCTION  (T) LTD.

error: Content is protected !!