CHAMA Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kinafanya mkutano mkuu wake leo Jumanne tarehe 4 Agosti 2020 katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam. Anaripoti Brightness Boaz…(endelea)
Wajumbe wa mkutano huo wameanza kuingia ukumbini kuhudhuria mkutano huo utakaojadili masuala mbalimbali kikiwemo kuwathibitisha Tundu Lissu kuwa mgombe urais wa Tanzania, Salumu Mwalimu, mgombea mwenza.
Pia, mkutano huo, utathibitisha Said Issa Mohamed kuwa mgombea urais wa Zanzibar katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020.
Lissu alipendekezwa jana Jumatatu na wajumbe wa Baraza Kuu la Chadema kwa kura 405 kati ya 442 sawa na asilimia 91 huku Lazaro Nyalandu akipata kura 36 na Dk. Mayrose Majinge akiambulia kura moja.
Pia, mkutano huo mkuu utakaoongozwa na Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema, utaipitisha Ilani ya Uchaguzi Mkuu wa chama hicho.
Kinachoendelea kwa sasa ukumbini ni wajumbe kuendelea kuwasili na wengine kuserebuka mziki unaopigwa na bendi.
Endelea kufuatilia MwanaHALISI Online, MwanaHALISI TV na mitandao yetu ya kijamii kwa habari na taarifa mbalimbali ya kinachoendelea
Leave a comment