Saturday , 27 April 2024
Home Habari Mchanganyiko TPA wafanya mageuzi uwekezaji wa vifaa kazi
Habari Mchanganyiko

TPA wafanya mageuzi uwekezaji wa vifaa kazi

Spread the love

 

MAMLAKA ya Bandari nchini (TPA), imefanya mageuzi makubwa ya uwekezaji kwenye vifaa vya kazi ambao, ukikamilika utakuwa na thamani ya sh bilioni 500. Anaripoti Mwandishi  Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Vifaa hivyo ambavyo tayari  vimeshaanza kuwasili, vitaingizwa nchini kwa awamu na awamu ya kwanza yenye  vifaa  vya thamani ya sh bilioni 210, vitakuwa vimekamilika ifikapo Juni 2022.

Akizungumza katika hafla ya kuzindua vifaa hivyo vya kazi bandarini leo tarehe 4 Novemba, 2021, Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Eric Hamissi amesema ujio wa  vifaa hivyo umeiingiza  Bandari katika moja ya matukio makubwa ya kihistori  nchini.

Amesema maboresho ya miundombinu yanayoendelea kufanywa, yanaleta changamoto ya uhitaji mkubwa wa vitendea kazi vya kisasa ili kuifanya Bandari kuwa na ufanisi wa viwango vya kimataifa na kuvutia zaidi wateja wa ndani na nje ya nchi.

“Bandari ya Dar es Salaam na tukio la leo linaandika rekodi ya kipekee na linaingia katika matukio ya kihistoria ya Bandari ya Da es Salaam na Bandari zote za TPA. Vifaa hivi na maboresho yaliyofanyika, yataongeza ufanisi, yataongeza mapato, sioni sababu ya kutofikia lengo la makusanyo ya sh trilioni moja,” amesema Eric.

Katika hafla hiyo ambayo mgeni rasmi amekuwa Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa, Eric amevitaja vifaa vilivyowasili kuwa ni pamoja na Reach steakers (7) mpya, kila moja ikiwa na uwezo wa kunyanyua tani 45.

Vifaa vingine ni boti tatu mpya za kuongozea meli (Pilot Boats) na kreni kubwa moja ya kubeba mizigo mchanganyiko.

“Mheshimiwa Waziri, vifaa hivi ni awamu ya kwanza ya vifaa mbalimbali vyenye thamani ya Shilingi Bilioni 210 ambavyo TPA iliviagiza kwa kufungua LC mwezi Juni 2021.

“Vitendea kazi vingine vitaendelea kuwasili kwa awamu hadi kufikia Mwezi Juni 2022 tutakapopokea RTG 2 na SSG 3 kama shehena ya mwisho kwa ajili ya Container terminal mpya berth 5 hadi 7,” alisema Hamis.

Mkurugenzi huyo alimpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuifanya TPA kutembea kifua mbele na kujiamini kutokana na uwezo ilionao hivi sasa ambao  ni matokeo ya uwezeshaji mkubwa uliofanywa na Serikali katika Sekta ya Bandari nchini, ikiwemo Bandari ya Dar es Salaam.

Katika kuhakikisha kuwa Bandari za Tanzania zinaendelea kutoa huduma bora kwa wateja wake, Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, imeendea kuziboresha bandari kwa kuzijengea uwezo wa kuhudumia meli na shehena kubwa zaidi,”

“Mheshimiwa Waziri, Mradi wa DMGP katika Bandari ya Dar es Salaam umefikia asilimia 98.Mradi huu utakapokamilika Juni Mwaka 2024, Bandari ya Dar es Salaam itakuwa na uwezo wa kuhudumia shehena ya tani milioni 25 kutoka tani milioni 16 za sasa.

Aidha, bandari hii itaweza kuhudumia meli zenye urefu wa mita 303 zinazoweza kubeba makasha hadi TEUS elfu 8. Kwa sasa, Bandari hii inahudumia meli zenye urefu wa mita 243 zinazoweza kubeba makasha hadi TEUS elfu 4.

Amesisitiza kuwa maboresho yote hayo ya bandari, hayawezi kuwa na maana kama hakutakuwa na vifaa  vya kisasa vya kutendea kazi.

Amesema awamu ya kwanza ya vifaa hivyo itagharimu sh bilioni 210, hivyo alimwomba Waziri Mbalawa kwamba watakapokuja maombi mapya kiasi kingine kilichosalia cha sh bilioni 290, wasisite kupewe.

Ametamba kuwa kwa maboresho ya bandari yanayoendelea kufanywa, uwepo wa  vifaa vya kazi pamoja  na wafanyakazi wenye ujuzi  na weledi, TPA itakuwa  na ufanisi mkubwa kuliko wakati mwingine wowote.

Amevisihi vyombo  vya habari kuandika mazuri ya bandari badala ya kuhangaika  na taarifa zingine ambazo nyingi ni za uzushi, uongo na zinachafua taswira njema ya bandari.

Ameshukuru ushirikiano TPA inaoupata kutoka kwa wadau wa sekta ya Bandari, Tasisi za Serikali, Sekta Binafsi kama vile TPSF, TSC, TASAA, TAFFA,Wenye Meli na Wasafirishaji wote kwa ujumla na vyombo vya habari.

Kwa upande wake, Waziri Mbarawa alisema kuwa kuwasili kwa vitendea kazi hivi ni mwendelezo wa mageuzi makubwa yanayofanyika TPA.

Waziri Mbarawa amesema mageuzi makubwa ya miundombinu katika Bandari, yamezalisha mahitaji makubwa ya vitendea kazi ili kuongeza ufanisi wa kuhudumia shehena kwa wakati unaokubalika.

“Rai yangu kwa Menejimenti ya TPA ni kuhakikisha kuwa, vifaa hivi vyenye thamani kubwa vinatunzwa, vinafanyiwa matengenezo kwa muda muafaka na kuendeshwa na watumishi wenye weledi wa kutosha, walioajiliwa ili viweze kudumu,” alisema.

Baadhi ya viongozi waliohudhuria hafla hiyo ni pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Jokate Mwigelo ambaye amemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makala.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Polisi wakanusha kufanya uzembe ajali iliyouwa mwandishi Ayo Tv

Spread the loveJESHI la Polisi limekanusha tuhuma zilizoibuliwa dhidi yake  kwamba limekawia...

Habari Mchanganyiko

Rais Samia kuzindua gazeti litakalotoa habari za wafanyakazi Tanzania

Spread the loveSHIRIKISHO la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), liko mbioni kufufua...

Habari Mchanganyiko

GGML yaja na teknolojia za kisasa maonesho ya OSHA Arusha

Spread the loveKATIKA kuelimisha wananchi na washiriki wa maonesho ya usalama na...

Habari Mchanganyiko

GGML, OSHA wawanoa mama lishe 50 kukabiliana na majanga ya moto

Spread the loveKampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) kwa kushirikiana na...

error: Content is protected !!