PETER Kibatala, Wakili wa utetezi katika kesi ya uhujumu uchumi yenye mashtaka ya ugaidi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake, amembana shahidi wa saba wa Jamhuri, Inspekta Mahita Omari Mahita, kuhusu matukio ya uhalifu yaliyokuwa yanafanywa na aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).
Kibatala amembana Inspekta Mahita ambaye alikuwa Msaidizi wa Mkuu wa Upelelezi wa Wilaya ya Arusha, leo Ijumaa, tarehe 5 Novemba 2021, katika Mahakama Kuu, Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, Mawasiliano jijini Dar es Salaam, mbele ya Jaji Joackim Tiganga.
Wakili Kibatala alimbana Inspekta Mahita baada ya kutoa ushahidi wake mahakamani hapo, uliodai yeye na wenzake walipokea maelekezo kutoka kwa aliyekuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoa wa Arusha (RCO), ACP Ramadhan Kingai ya kuzuia kundi linalodaiwa kuandaliwa na Mbowe, ili kufanya vitendo vya ugaidi.
Pia, kundi hilo linadaiwa kutaka kulipua vituo vya mafuta na kudhuru viongozi wa serikali akiwemo Sabaya.
Kwa sasa, Sabaya anatumikia kifungo cha miaka 30 gerezani baada ya kukutwa na hatia ya unyang’anyi wa kutumia silaha pamoja na wenzake. Pia, kesi nyingine na wenzake sita ya kuendesha kundi la kihalifu inaendelea mahakamani Arusha.
Katika moja ya maswali aliyoulizwa na Kibatala ni suala la uhalifu uliokuwa ukifanywa na Sabaya wakati yeye Inspekta Mahita ambaye ni mtoto wa Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) mstaafu Omar Mahita akiwa msaidizi wa mpelelezi.
Mahoajino ya Kibatala na shahidi huyo yalikuwa hivi;
Kibatala: Unafahamu kwamba Sabaya aliyekuwa Mkuu wa Wilaya amehukumiwa na Mahakama kwa Makosa ya Ujambazi
Shahidi: Ndiyo nafahamu
Kibatala: Je unafahamu kwamba Sabaya amehukumiwa makosa ya ujambazi wakati wewe ukiwa afisa wa polisi Arusha na ACP Kingai
Shahidi: Ndiyo natambua
Kibatala: Wewe ulifanya jukumu gani katika kuzuia uhalifu wa Sabaya
Shahidi: Siyo lazima mimi lakini kuna wasaidizi waliopo chini yangu walizipata
Kibatala: Na unafahamu kwamba matendo yake yalijirudia rudia
Shahidi: Sifahamu
Kibatala: Mwambie mheshimiwa Jaji iwapo wewe na afande Kingai kama mlipata taarifa za intelijensia kuhusu uhalifu wa Sabaya
Shahidi: Sikupata taarifa
Kibatala: Lakini unajua mipango ya uhalifu wa wilaya ya Hai, nje ya eneo lako la kazi
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Kwanini tusiseme kwamba kesi hii nyinyi na Sabaya mlitengeneza kesi kwa ajili ya mambo ya Kisiasa
Shahidi: Siyo kweli kabisa
Kibatala: Huyu ASP Jumanne yupo wapi
Shahidi: Yupo Arumeru
Kibatala: Kwamba ufahamu kwamba Jumanne amesimamishwa kazi baada ya kumbambikia Mzee mstaafu kuwekewa meno ya tembo kwenye mzinga wake wa nyuki chini ya usimamizi wa ASP Jumanne ambaye ni shahidi wenu
Shahidi: Sifahamu najua yupo kazini
Kibatala: Muda huu tunapo ongea yupo ofisini?
Shahidi: Sifahamu kwa sababu siwasiliani naye siku nyingi
Kibatala: Na unajua tukio lake la kusimamia kumuwekea mzee wa watu meno ya tembo
Shahidi: Nafahamu
Kibatala: Je, ukimfahamisha huyu aliyetoka Kudhuliwa Sabaya
Shahidi: Sijamwambia
Kibatala: Ulimwambia mheshimiwa Jaji kwamba uliifahamisha kamati ya ulinzi ya wilaya Hai au Mkoa wa Kilimanjaro
Shahidi: Hapana Siku Mwambia
Kibatala: Katika briefing zenu, Je Kingai aliwambia kwamba ametoa taarifa kwa kati za ulinzi na usalama
Shahidi: Hakutuambia
Leave a comment