Saturday , 27 April 2024
Home Habari Mchanganyiko TMA tangaza utabiri wa msimu wa mvua za Mwaka, watoa ushauri
Habari Mchanganyiko

TMA tangaza utabiri wa msimu wa mvua za Mwaka, watoa ushauri

Mkurugenzi wa Huduma za Utabiri wa TMA, Dk. Hamza Kabelwa
Spread the love

MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetangaza utabiri wa Msimu wa Mvua za Mwaka unaotarajiwa kuanza mwezi Novemba 2022 na kumalizika Aprili 2023, ambapo mikoa 14 inayopata msimu mmoja wa mvua inatarajiwa kunyesha mvua za chini ya wastani hadi wastani. Anaripoti Erasto Masalu, Dar es Salaam … (endelea).

Utabiri huo umetangazwa leo tarehe 26 Oktoba, 2022 na Mkurugenzi wa Huduma za Utabiri wa TMA, Dk. Hamza Kabelwa ambapo amesema mwelekeo wa mvua za msimu kwa maeneo yanayopata msimu mmoja wa mvua kwa mwaka mikoa inayotarajiwa kupata mvua hizo ni Kigoma, Tabora, Katavi, Singida, Dodima, Ruvuma na Lindi.

Mikoa mingine ni Lindi, Mtwara, Njombe, Rukwa, Songwe, Mbeya, Iringa na kusini mwa Morogoro.

Amesema kunyesha kwa mvua hizo chini ya wastani imesababishwa na La Nina ambapo kutakuwa na joto la bahari la chini ya wastani katika eneo la kati la bahari ya Pasifiki linatarajiwa kuendelea kuwa chini ya wastani.

Dk. Kabelwa amesema katika nusu ya kwanza ya msimu kuanzia Novemba mwaka 2022 hadi Januari mwaka 2023 vipindi virefu vya ukavu vinatarajiwa kujitokeza.

“Ongezeko la mvua linatarajiwa katika nusu ya pili ya msimu kuanzia Februari hadi Aprili mwaka 2023 na mvua za nje ya msimu zinatarajiwa kunyesha Mei mwaka 2023 katika maeneo mengi,” amesema Dk. Kabelwa.

Dk Kabelwa amesema athari zinazotarajiwa kujitokeza upungufu mkubwa wa unyevunyevu katika udongo katika maeneo hayo yanayopata mvua hizo na kuathiri ukuaji wa mazao na upatikanaji wa malisho kwa ajili ya mifugo

Amesema athari zingine zinazotarajiwa kujitokeza kina cha maji katika mito na mabwawa kinatarajiwa kupungua na kuathiri upatikanajibwa maji kwa matumizi mbalimbali kama vike umwagiliaji na uzalishaji wa nishati.

Dk Kabelwa amezisahuri mamlaka kuhakikisha vyanzo vya maji vinatunzwa pamoja na kuweka miundombinu ya uvunaji maji na kuandaa na kutekeleza mipango mkakati ya kuhimiza kilimo himilivu.

“Hali hii inaweza kuathiri uoteshaji na ukuaji wa mazao hususan katika kipindi cha Novemba na Desemba 2022 kutakuwa na ongezeko la bisumbufu vya mazao kama vile mchwa,viwavijeshi ,panya vinatarajiwa kujitokeza katika msimu na kuarhiri mazao ya uzalishaji kwa ujumla pamoja na matukio ya moto yanaweza kujitokeza kutokana na vipindi virefu vya ukavu vinatarajiwa,” amesema Dk. Kabelwa.

Amesema wakulima wanatakiwa kupanda mazao na mbegu zinazokomaa kwa muda mfupi na zinazostahimi upungufu wa mvua kama vile mihogo,viazi mikunde na mazaobya bustani.

Pia katika upatikanaji wa maji na malisho kwa ajili ya mifugo na kupelekea uwezekano wa migogoro kujitokeza baina ya wafugaji na watumiaji wengine wa ardhi.

Naye Mtabiri wa Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Joyce Makwata amesema matukio ya vipindi vya mvua kubwa yanaweza kujitokeza hata katika maeneo yanayotarajiwa kupata mvua chini ya wastani.

“Upi uwezekano wa kutokea kwa migandamizo midogo ya hewa kusini magharibi mwa Bahari ya Hindi ikiwa ni pamoja na rasi ya Msumbiji hivyo kusababisha vipindi vya mvua katika nusu ya pili ya msimu,”amesema Makwata.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!