Wednesday , 8 February 2023
Home Kitengo Michezo Nyota wanne Simba kuikosa Azam kesho
Michezo

Nyota wanne Simba kuikosa Azam kesho

Juma Mgunda
Spread the love

KLABU ya Soka ya Simba inatarajiwa kuwakosa nyota wake wanne kuelekea mchezo wa kesho tarehe 27 Oktoba 2022 ambapo Simba watakuwa wageni wa Azam FC katika mchezo Ligi Kuu Bara utakaofanyika kwenye dimba la Benjamin mkapa jijini Dar es salaam Simba. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Simba itawakosa Sadio Kanoute, Israel Mwenda, Mzamiru Yassin na Jimmsony Mwanuke katika mchezo huo ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

Hayo yamebainishwa leo tarehe 26 Oktoba, 2022 na Kocha mkuu wa Simba, Juma Mgunda wakati akizungumza waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuelezea maandalizi ya mchezo huo.

Amesema mandalizi ya mchezo yamekamilika na tayari walishajiandaa tangu walipokuwa katika maandalizi kabambe ya kumenyana na mtani wao Yanga.

Amesema katika mechi hiyo watamkosa Kanoute ambaye ni mgojwa, Israel Mwenda aliyeumia kwenye mchezo wa Jumapili dhidi ya Yanga, pia watamkosa Jimmyson Mwanuke ambaye ni majeruhi wa siku nyingi wakati kiungo wao Mzamiru Yassin atakosekana kutokana na kuzawadiwa kadi tatu za njano.

Aidha, kocha huyo alielezea kurejea kwa beki kisiki wa timu hiyo Shomari Kapombe ambaye ameshaanza mazoezi na wenzie akitoka kuuguza majeruhi huku wachezaji wengine wakiwa tayari kwa ajili ya mchezo huo mgumu dhidi ya Azam.

“Tujua ugumu wa mchezo Azam, tunawaheshimu ni timu nzuri na wanacheza kitimu hivyo kuzingatia ugumu wa mchezo maandalizi tulianza mapema,” amesema Mgunda.

Aidha, kwa upande wa Azam, Kocha mkuu wa muda wa timu hiyo, Kali Ongala amesema kuwa wao wamejiandaa kwa ajili ya mchezo huo kwani wanaamini michezo yote ni migumu.

Amesema licha ya kutokuwa na kiwango bora sasa hali inayosababisha timu kutopata matoke, bado wanaamini watapambana kupata matokeo mazuri ambayo yatawafanya kusogea nafasi za juu na kuwakaribia waliowatangulia.

Aidha, amempongeza kocha Mgunda kwa mafanikio aliyopata kwa muda mfupi hasa ikizingatiwa ni kocha mzawa jambo ambalo linawapa motisha wao kama makocha wazawa kuamini kuwa kila kitu kinawezekana.

Mchezo huo unakuwa wa kwanza kwa timu hizi kukutana kwa msimu huu ambapo mpaka sasa Simba wapo nafasi ya pili wakiwa na pointi 14 na faida ya magoli tisa katika michezo sita waliyocheza mpaka sasa.

Kwa upande wa Azam wapo nafasi ya nane na pointi zao 11 pamoja na faida ya goli moja katika michezo saba waliyocheza mpaka sasa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

GGML: Uwanja mpya wa Geita Gold FC kukamilika Mei, 2023

Spread the loveUWANJA wa Magogo unaojengwa na Halmashauri ya Mji wa Geita...

Michezo

Wanafunzi chuo Mwalimu Nyerere wapongezwa kwa ushindi

Spread the love  UONGOZI wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA)...

Michezo

Arsenal waipopoa Manchester United

Spread the loveKLABU ya Arsenal inayoshiriki Ligi Kuu England imewatandika Mashetani Wekundu...

Michezo

Mchezaji Singida apoteza maisha mazoezini

Spread the love  MCHEZAJI na kapteni wa timu ya vijana ya Singida...

error: Content is protected !!