Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari TLS yazungumzia utawala wa sheria, Spika Tulia ajibu
Habari

TLS yazungumzia utawala wa sheria, Spika Tulia ajibu

Dk. Tulia Ackson, Spika wa Bunge la Tanzania
Spread the love

 

CHAMA cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS), kimeshauri wananchi washirikishwe kikamilifu katika michakato ya utungwaji sheria, kwani jambo hilo linawafanya waridhie mfumo wa sheria. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Wito huo umetolewa leo Jumatano, tarehe 2 Februari 2022 na Rais wa TLS, Profesa Edward Hoseah, akizungumza katika kilele cha maadhimisho ya siku ya sheria nchini Tanzania, yaliyofanyika jijini Dodoma ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Rais Samia Suluhu Hassan.

“Utawala wa sheria unawezesha wananchi washiriki katika utungwaji sheria na kuridhia mfumo mzima wa sheria, hivyo utawala wa sheria huwafaanya watu waifahamu sheria kupitia rogram mbalimbali za uendeshaji umma hata kama hawana utaalamu wa sheria hizo,” amesema Prof. Hoseah.

Wakati huohuo, Profesa Hoseah ameishauri mihimili kushirikiana katika kuwaletea maendeleo Watanzania.

“Hakuna kati yetu aliye juu ya sheria na kwamba kuna mgawanyo wa mihimili ya dola, dhana hiyo ndiyo inayoleta heshima ya kuheshimu sheria, hata hivyo haina maana kwamba mihimili sisihirikiane kwa dhamira ya kuwaletea maendeleo wananchi na kupata haki zao stahiki,” amesema Profesa Hoseah

Aidha, Profesa Hoseah aliyewahi kuwa mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), alivishauri vyombo vya maamuzi vifuate utawala wa sheria katika utekelezaji wa majukumu yake.

“Katika kuhakikisha utawala wa sheria unafuatwa na kunafanya kazi, mifumo yote ya utoaji haki lazima ifuate utaratibu uliowekwa katika kutoa haki, ili kuhakikisha utekelezaji wa kufuata utaratibu huu. Ni muhimu na vyombo vyote muhimu kushiriki na kupokea ushauri,” amesema Profesa Hoseah na kuongeza:

“Wa utekelezaji wa jambo husika kutoka katika makundi yote ya kisheria na hata ya kijamii yanayoweza kutoa ushauri wa kisheria. La msingi ambalo nalisisitiza ni utu wa mtu unasisitizwa katika utoaji haki na kutekeleza dhana ya utawala wa sheria.”

Akijibu ushauri wa wananchi kushirikishwa katika utungaji sheria, Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson amesema wananchi wanashirikishwa kikamilifu katika mchakato huo.

“Nimtoe wasiwasi yeye lakini pia niwatoe wasiwasi wananchi, utaratibu wa kutunga sheria sisi kama watunga sheria ni wawakilishi wa wananchi wa nchi hii. Lakini kwa kutambua kwamba sisi ni wachache, wananchi ni wengi na TLS ni sehemu ya watu ambao huwa tunawaita kama wadau kushiriki katika mchakato,” amesema Dk. Tulia.

Dk. Tulia amesema “wakati ambapo tunaletewa miswada bungeni na Serikali, kwa hiyo Rais wa TLS usiwe na wasiwasi ukifuatilia vizuri kwenye chama chako utagundua kwamba, ninyi ni washiriki wazuri.”

Spika huyo wa Bunge, ametoa wito kwa wananchi na wadau wa sheria pindi Bunge linapotoa tangazo la kukusanya maoni juu ya mapitio ya miswada ya Sheria, kuitumia fursa hiyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

HabariSiasa

Dk. Rose Rwakatare atoa kadi 500 kila Wilaya Morogoro

Spread the loveMWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Morogoro, Dk...

ElimuHabari

CBE, WMA wasaini makubaliano wanafunzi kusoma wakifanyakazi

Spread the loveNAIBU Spika Musa Azzan Zungu amekipongeza Chuo cha Elimu ya...

HabariTangulizi

Dk. Slaa, Mwabukusi kuhojiwa na jeshi la Polisi Mbeya

Spread the loveJESHI la Polisi jijini Mbeya, linawashikilia kwa mahojiano Dk. Wilbroad...

HabariHabari Mchanganyiko

Kairuki Hospital Green IVF  yawanoa madaktari kuhusu upandikizaji mimba

Spread the love KITUO cha Upandikizaji Mimba cha Kairuki Hospital Green IVF...

error: Content is protected !!