MAPINDUZI yameripotiwa katika nchi ya Afrika Magharibi ya Guinea-Bissau, yamesababisha vifo vya maafisa kadhaa wa vikosi vya usalama, rais wake anasema. Inaripoti mitandao ya kimataifa…(endelea).
Umaro Cissoko Embaló alisema, hali imedhibitiwa nakuitaja kuwa “kushindwa kwa mashambulizi dhidi ya demokrasia.”
Makabiliano ya risasi yalizuka karibu na jengo la serikali Jumanne ya tarehe 1 Februari 2022 katika mji mkuu wa Bissau ambapo rais aliripotiwa kuhuduria mkutano wa Baraza la Mawaziri.
Watu wasiojulikana waliokuwa na silaha nzito walishambulia Ikulu ya serikali wakati Rais Embaló alipokuwa akikutana na Waziri Mkuu, Nuno Gomes Nabiam, kulingana na ripoti kutoka eneo la tukio.
Shirika la utangazaji la BBC, limenukuu vyanzo mbalimbali vya taarifa vikisema, wanaume waliokuwa wamejihami kwa bundukiwa wakiwa wamevalia nguzo za nyumbani, walimpiga risasi na kumuua afisa wa polisi.
Umaro Sissoco Embaló, alichaguliwa kuwa rais mwaka 2019.
Viongozi wa Kanda ya Afrika Magharibi walielezea tukio hilo kama jaribio la mapinduzi na kuwataka wanajeshi kurejea kwenye kambi.
Lakini kilichotokea bado hakijabainika. Bado haijajulikana mtu aliyejihami ni nani na rais hakutoa idadi kamili ya waliouawa.
Nchi hiyo masikini na koloni la zamani na Ureno, imeshuhudia mapinduzi tisa au majaribio ya mapinduzi tangu mwaka 1980.
Leave a comment