Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa TCD kujadili mgomo wa Chadema
Habari za SiasaTangulizi

TCD kujadili mgomo wa Chadema

Zitto Kabwe, Kiongozi wa ACT Wazalendo na Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD)
Spread the love

 

KITUO cha Demokrasia Tanzania (TCD), kimesema kitajadili sababu za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kugoma kushiriki kongamano lake la amani, linalotarajiwa kufanyika mwishoni mwa Machi, 2022, jijini Dodoma ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais Samia Suluhu Hassan. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa kutoka ndani ya kituo hicho, zinaeleza kwamba Kamati ya Ufundi ya TCD, hivi karibuni itaketi kujadili sababu hizo, ili kupata muafaka wake.

“Kila kituo kinapoitisha mkutano kamati ya ufundi inakutana na moja ya ajenda itakuwa kujadili hilo kongamano, katika kujadili itatazamwa mafanikio na changamoto. Kwenye changamoto utaona mwanachama mmoja hawezi kushiriki, kwa hiyo maazio yatatolewa,” amesema Afisa kutoka TCD ambaye hakutaka kutaja.

Aidha, afisa huyo wa TCD amesema kama majadiliano hayo hayatazaa matunda, vyama wanachama wa kituo hiko walio tayari kushiriki watashiriki kongamano hilo, ikiwemo na vyama vingine vya siuasa visivyokuwa wanachama wake ambao wamealikwa.

“TCD inaundwa katika utaratibu wa maridhiano, vikao vinavyohusika vitaendelea kujadili jambo hili kutafuta muafaka, ikifika mwisho hatujapata majawabu na wadau wengi wameonesha nia ya kushiriki, tutaenda kwenye kongamano,” ameesema afisa huyo.

Chama cha Chadema, mwishoni mwa wiki iliyopita kupitia Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe, kilisema hakitashiriki kongamano hilo, huku miongoni mwa sababu zao zikidai hawaoni nia njema kuhusu mjadala wa upatikanaji katiba mpya.

Pia, Mbowe alidai chama chake kimepitia ratiba ya kongamano hilo, na kuona baadhi ya watoa mada wake, ni wale walioshiriki mchakato wa Uchaguzi Mkuu wa 2020, ambao waligoma kutambua matokeo yake wakidai hayakuwa halali.

1 Comment

  • Zitto,
    Watu wanasema wewe ndiye tatizo. Unatanguliza hoja zako na wengine uwatakao na kuinyima CHADEMA.
    CCM tunaungana wakati wa siasa na kutofautiana wakati usio wa siasa.
    Nyiye wapinzani mnatofautiana wakati wa siasa halafu mnaungana wakati usio wa siasa.
    Bila UKAWA nyie mlie tu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

error: Content is protected !!