May 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mabadiliko Katiba, tume huru: LHRC watoa mapendekezo 14

Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Anna Henga

Spread the love

 

KITUO cha Sheria na Haki za Binadamu nchini (LHRC), kimetoa mapendekezo 13 kwa Kikosi Kazi cha Kiratibu Maoni ya Wadau wa Demokrasia ya Vyama vya Siasa, kwa ajili ya kutumika katika maboresho ya katiba na tume huru ya uchaguzi. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Mapendekezo hayo yametolewa leo Jumanne, tarehe 22 Machi 2022, jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Anna Henga, siku moja baada ya Rais Samia Suluhu Hassan, kuomba apewe mapendekezo kwa ajili ya kufanya marekebisho ya katiba na tume huru ya uchaguzi.

“Wakati Rais akihutubia Taifa katika hafla ya kupokea ripoti hiyo, ameagiza kikosi kazi kuja na mapendekezo yanayohitaji mabadiliko ya sheria ya haraka ya sheria na katiba, hivyo LHRC ikiwa mdau muhimu wa demokrasia na utawala bora inapenda kutoa mapendekezo kwa kikosi kazi hicho,” amesema Henga.

Henga ametaja mapendekezo hayo kuwa ni, sheria zisiruhusu Jeshi la Polisi kutoingilia shughuli za vyama vya siasa, wakati, kabla na baada ya kampeni, kinyume cha sheria, huku lingine likiwa ni uwepo wa wagombea binafsi kwenye ngazi mbalimbali za uchaguzi.

“Kuruhusu mgombea binafsi itasadidia kupunguza urasimu wa vyama vya siasa ambavyo hutumia sifa ya uanachama dhidi ya wagombea ikitokea kutoelewana baina ya pande hizo mbili. Pia kuendana na maamuzi ya Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu Afrika,” amesema Henga.

Mapendekezo mingine ni urekebishaji wa namna ya upatikanaji watumishi wa tume ya uchaguzi, ambao utawaondoa wakurugenzi wa halmashauri zote nchini kuwa wasimamizi wa uchaguzi katika ngazi za jimbo na mkurugenzi wa uchaguzi, mwenyekiti wa tume ya uchaguzi, pamoja na makamishna wapatikane kwa kuomba kazi ambazo zitatangazwa hadharani.

“Pendekezo lingine ni uteuzi wa wajumbe wa tume ya uchaguzi uzingatie uwakilishi wa vyama vikubwa vya siasa, asasi za kiraia, taasisi za dini na wanataaluma. Kigezo cha kupita bila kupingwa kiondolewe, hata kama mtu atapita bila kupingwa kuwe na kura ya ndiyo au hapana,” amesema Henga.

Rais Samia Suluhu Hassan

Mapendekezo mengine ya kituo hicho ni uwepo wa mifumo ya kielektroniki wa kupiga kura, uwepo wa takwa la kisheria kwa vyama vya siasa kuzingatia usawa wa kijinsia na watu wenyewe ulemavu na mikutano ya hadhara ifanyike kwa usawa kwa vyama vyote.

Pia, LHRC kimependekeza nafasi ya msajili wa vyama vya siasa iwe ya kutangazwa na kuombwa hadharani kwa vigezo vitakavyoanishwa na kamati maalumu ya kuajiri huku la mwisho likiwa ni kurekebisha sheria ya vyama vya siasa na kuondoa marekebisho yaliyofanyika 2019, ambayo yalirudisha nyuma ustawi wa demokrasia ya vyama vingi nchini.

error: Content is protected !!