Friday , 29 September 2023
Home Habari Mchanganyiko TARURA yajipa jukumu kutafutia kazi watoza ushuru magari
Habari Mchanganyiko

TARURA yajipa jukumu kutafutia kazi watoza ushuru magari

Spread the love

WAKALA wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA) Mkoa wa Mwanza, umewataka wakusanya ushuru wa maegesho ya magari waliokosa nafasi za kazi kujiunga katika vikundi vidogo vidogo ili kunufaika. Anaripoti Moses Mseti, Mwanza … (endelea).

Ni kujiunga katika mfumo mpya wa kielektroniki wa ukusanyaji ushuru wa maegesho ya magari na kwamba, TARURA wameamua kuwatafutia fursa nyingine baada ya kuanza kutumika kwa mfumo mpya wa kielektroniki wa ukusanyaji wa ushuru wa maegesho wa magari.

Mhandisi Kuyoya Fuko, Mratibu wa Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (Tarura) Mkoa wa Mwanza, ametoa kauli hiyo leo tarehe 2 Mei 2019 wakati akizungumza na mwandishi wetu ofisini kwake.

Mwandishi alitaka kujua kuhusu kuanza kwa mfumo huo mpya na wa kisasa wa ukusanyaji wa ushuru wa maegesho wa magari jijini Mwanza.

Fuko amesema, baada ya kuanza kwa mfumo huo, kumekuwepo na baadhi ya watu kuanzisha migogoro ya kutaka kukwamisha mipango ya serikali ya kukusanya kodi kwa njia rahisi na salama.

Amesema, serikali inakuja na mfumo huo wenye lengo la kuokoa fedha za umma zilizokuwa zinapigwa na baadhi ya watu wachache, ambap serikali imekuwa ikikosa fedha nyingi na kushindwa kukamilisha miradi ya maendeleo.

“Kuna taarifa kwamba, viongozi wa TARURA wameweka wakusanya ushuru wao na kwamba, wale wa zamani wameondolewa kwa njia ambazo sio sahihi.

“Sasa ninachotaka kusema huo ni uongo na hakuna kitu kama hicho, na watu wote walifanyiwa usaili na wale ambao wamekosa hawakukidhi vigezo,” amesema.

Mhandisi Fuko amedai kuwa, wakusanya ushuru wa zamani walio ondolewa, tayari wamewaelekeza namna ya kujiunga katika vikundi vidogo vidogo kwa ajili ya kufanya kazi ndogondogo ikiwemo kufyeka majani na kusafirisha mitaro pindi inapohitajika.

“Sisi lengo letu ni zuri na huu mfumo mpya una manufaa makubwa, ukiangalia Mwanza mjini kwa siku gari zinazopaki ni zaidi ya 5000, lakini kiasi cha fedha tulichokuwa tukikipata ni kidogo ukilinganisha na idadi ya gari.

“Tumejiwekea lengo la kukusanya kiasi cha fedha kisichopungua Sh. Milioni 58 kwa mwezi, lakini kwenye majaribio ya awali ambayo tumefanya tumevuka lengo tumekusanya Sh. Milioni 100 kwa mwezi,” amesema Mhandisi Fuko.

Happnes Kyaruzi, mmoja wa wakusanya ushuru wa maegesho wa magari jijini Mwanza, kupitia mfumo huo mpya, amesema Kampuni ya NPK Tecknologies iliyopewa mamlaka ya kusimamia ukusanyaji ushuru wa maegesho ya magari jijini Mwanza, iliendesha usaili kwa watu wote huku akidai kuna ambao walifanikiwa kuchaguliwa katika usaili na wengine kuachwa.

Katibu wa Kampuni ya NPK Technologies, Desderius Kabashi alipotafutwa kuzungumzia suala hilo, alidai hakuna hujuma ambazo zimefanywa katika usaili wa wakusanya ushuru hao na kwamba, kila kitu kilikuwa kwa wazi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Stamico yafungua fursa za kiuchumi kwa makundi maalumu

Spread the loveSHIRIKA la Madini la Taifa (STAMICO) limemwaga neema kwa watu...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Maabara ya bilioni 5 upimaji madini yazinduliwa Geita, inapima kwa mionzi

Spread the loveZaidi ya Sh bilioni tano zimewekezwa katika kampuni ya MSALABS...

ElimuHabari Mchanganyiko

Wanafunzi Nyamkumbu wanolewa na GGML kuhusu taaluma ya madini

Spread the loveZAIDI ya Wanafunzi 50 kutoka Shule ya Sekondari ya Wasichana...

Habari Mchanganyiko

Makamba: China ni ya mfani kwa kupunguza umaskini

Spread the loveWAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, January...

error: Content is protected !!