December 9, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Ratiba ya Msiba wa Dk. Mengi kesho, Makonda, Rungwe watoa neno

Spread the love

RATIBA ya Msiba wa Reginald Mengi, Mkurugenzi wa Kampuni  za IPP zitafahamika kesho saa saba mchana. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Akizungumza na Waandishi wa Habari nyumbani kwa marehemu, Michael Ngalu,  Mwanasheria na Msemaji wa Familia hiyo amesema kuwa kesho saa 7 mchana familia itatoa ratiba ya mazishi ya msiba huo.

Wakati huohuo wanasiasa kadhaa walifika kwenye msiba huo na kueleza namna walivyoguswa na msiba huo.

Hashimu Rungwe, Mwenyekiti wa Chama Cha Ukombozi wa Umma (Chaumma), amesema kuwa msiba wa Dk. Mengi umeligusa taifa na kwamba marehemu alikuwa rafiki wa kila mtu.

Amesema kuwa kwa upande wake hakumuona Dk. Mengi akiwa mbaguzi wa kisiasa wala dini alisaidia watu wote.

Paul Makonda, Mkuu wa Mkoa  wa Dar es Salaam amesema kuwa taifa limepata pigo kufuatia msiba wa Dk. Mengi ambapo amekuwa na mchango kwa watu wengi nchini.

Amesema kuwa yeye na vijana wengine wengi walishikwa mkono na Dk. Mengi kwenye mchango wa kielimu na hata kifedha.

Amewatia moyo walemavu kuwa Mungu aliyemchukua Dk. Mengi atamleta mwingine atakayekamilisha lile aliloadhimia la kuwajengea kiwanda walemavu.

Abdallah Ambua, Mtangazaji wa East Afrika  Radio na Televisheni, amesema kuwa msiba huo ni mkubwa licha ya marehemu kuacha alama muhimu nchini kwa kuwafungulia milango ya fursa vijana, walemavu na wazee.

error: Content is protected !!