Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Tanzania kupokea mabilioni ya wafadhili
Habari za Siasa

Tanzania kupokea mabilioni ya wafadhili

Profesa Palamagamba Kabudi
Spread the love

SERIKALI ya Tanzania inatarajia kupokea fedha za msaada, kwa ajili ya kukabiliana na athari za mlipuko wa ugonjwa wa homa kali ya mapafu, inayosababishwa na virusi vya corona (Covid-19), Dola za Marekani 68 Mil (sawa na Sh. 156.4 bilioni), kutoka kwa wafadhili. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Hayo yamesemwa leo Alhamisi tarehe 21 Mei 2020 na Profesa Palamagamba Kabudi, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, katika hafla ya uapisho wa viongozi sita iliyofanywa na na Rais John Magufuli, Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma.

Mara baada ya Rais Magufuli kumaliza kuwaapisha viongozi hao, Profesa Kabudi alisema Umoja wa Ulaya (EU) umeahidi kuipa Tanzania Dola 38 milioni, wakati nchi ya Sweden ikiahidi kutoa dola 30 milioni katika mapambano ya corona.

“EU wameamua kutoa dola Mil. 38 ambazo zitakuja Tanzania kutusaidia katika maeneo mbalimbali baada ya hili janga kuisha. Lakini pia nimeongea na Sweden kwa njia ya mtandao wataongeza dola Mil. 20, katika bajeti ya elimu na dola Mil. 10 TASAF, ili zisaidie katika mapambano ya Covid- 19,” amesema Profesa Kabudi.

Profesa Kabudi amesema, Tanzania inashirikiana vyema na nchi wahisani katika mapambano dhidi ya Covid-19, lakini haiweki wazi taarifa hizo, kwa kuwa haifanyi mashindano kuhusu janga hilo.

“Hatuyasemei sana hadharani sababu ugonjwa huu sio ligi, kuonesha nani amefunga magoli mangapi, kazi inafanyika na tunakushuruku sana wakati wa vita, maelezo ya jemedali hayatakiwi kutafsiriwa bali kutekelezwa,” amesema Profesa Kabudi.

 Waziri huyo amesema, Tanzania inapongezwa na mataifa mbalimbali, kuhusu namna wanavyoshughulikia janga la Covid-19.

Amesema mataifa hayo yameahidi kuisaidia Tanzania katika kuimarisha uchumi na kupambana na Covid-19, kulingana na mikakati yake iliyojiwekea.

“Jana, nimepokea simu kutoka kwa waziri wa ushirikiano wa kimataifa wa Canada tuliongea jioni, wanatupongeza kwa hatua na wameahidi kutusiaidia katika eneo la elimu na afya kwa kadri mahitaji yetu yatakavyokuwa,” amesema Profesa Kabudi.

“Na nilimsisitizia sisi watupe pesa tutajua maeneo gani tutazipeleka katika kuimarisha uchumi na kupambana na maradhi haya.”

Viongozi walioapishwa ni; Dk. Godwin Mollel kuwa Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wanawake Wazee na Watoto.

Dk. Mollel ameapishwa kuchukua nafasi ya Dk. Faustine Ndungulile ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.

Dk. Delphine Magere ameapishwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani kuchukua nafasi ya Theresia Mbando ambaye amestaafu kwa mujibu wa utumishi wa umma.

Wengine ni; Dk. Jacob Kingu kuwa Balozi wa Tanzania nchini Algeria, Phaustine Kasike kuwa Balozi wa Tanzania nchini Msumbiji na John Simbachawene kuwa Balozi wa Tanzania nchini Kenya.

Pia, Rais Magufuli amemwapisha Brigedia Jenerali, John Mbungo kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa (Takukuru).

Hafla hiyo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwamo mawaziri na wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

error: Content is protected !!