MAAMBUKIZO ya ugonjwa unaosababishwa na virusi vya corona (COVID-19) yamefikia milioni 5.1 duniani huku vifo vikiwa 330,004. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).
Kwa mujibu ya mtandao wa Worldometer, hadi leo saa 7 mchana ya tarehe 21 Mei, 2020, kati ya wagonjwa hao milioni 5.1, waliopona ugonjwa huo ni milioni 2.03.
Marekani imeendelea kuongeza kwa idadi ya wagonjwa 1.59 milioni sanjari na vifo vikifikia 94,941huku waliopona wakiwa 370,812.
Urusi inashika nafasi ya pili duniani ikiwa na wagonjwa 317,554, vifo 3,099 na waliopona ni 92,681.
Brazili inawagonjwa 293,357, ikiwa nafasi ya tatu kwa wagonjwa wengine huku vigo vikiwa 18,894 na waliopona ni 116,683. Hispania ina wagonjwa 279,524, vifo 27,888 na waliopona ni 196,958.
Uingereza kuna wagonjwa 248,293 na vifo vikifikia 35,704. Nchi ya China ambako ndiko ugonjwa huo ulianzia mwishoni mwa mwaka 2019, ina wagonjwa 82,967, vifo 4,634 na waliopona ni 78,249.
Leave a comment