Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari Tanzania kujenga kiwanda chanjo UVIKO-19
HabariTangulizi

Tanzania kujenga kiwanda chanjo UVIKO-19

Spread the love

 

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema, Serikali anayoiongoza ina mpango wa kuanzisha kiwanda cha kuzalisha chanjo ya korona (UVIKO-19) na maradhi mengine ndani ya nchi. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Amesema hayo jana Jumanne, tarehe 15 Februari 2022, alipofanya mazungumzo na Charles Michel, Rais wa Baraza la Umoja wa Ulaya wakati wa ziara yake rasmi nchini Ubelgiji.

Taarifa iliyotolewa na Zuhura Yunus, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu imeeleza kwamba, Rais Samia amesema bajeti ya Serikali ya Tanzania kununua chanjo inakadiriwa itaongezeka kutoka Sh.26.1 bilioni mwaka 2020 hadi Sh.216 bilioni, ambayo ni sababu muhimu ya kujenga kiwanda hicho.

“Tanzania inaomba kuwasilisha mapendekezo, natarajia mtawezesha wazo hili kuwa mradi wenye manufaa. Naamini mpango huu utakapotekelezwa utafungua fursa mpya za kuimarisha mahusiano yetu,” amesema Rais Samia

Tangu kuanzishwa rasmi kwa ushirikiano mwaka 1975, Tanzania imepokea zaidi ya Euro bilioni 2.3 ambayo ni sawa nba Sh.5.98 trilioni. Tangu wakati huo, Umoja wa Ulaya umebaki washirika wa kimkakati na wa kimaendeleo kwa Tanzania.

Wakati huohuo, Rais Samia ameusihi Umoja wa Ulaya kuendelea kuunga mkono jitihada za Serikali ya nchi jirani ya Burundi kuimarisha mazingira ya ndani na nje ya nchi, akisisitiza umoja huo una ushawishi mkubwa hata kwa jumuiya nyingine za kimataifa kuunga mkono jitihada za kuleta utulivu na maendeleo.

“Burundi tulivu ina manufaa kwa maeneo ya maziwa makuu, nzuri kwa Umoja wa Ulaya na duniani kwa jumla,” amesema Rais Samia

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za SiasaTangulizi

Shibuda amlima waraka mzito Bulembo

Spread the loveMKONGWE wa siasa nchini, John Shibuda amemshukia kada maarufu wa...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia ataja mikakati ya kufikia trilioni 2 biashara Uturuki, Tz

Spread the loveWakati Tanzania na Uturuki zikidhamiria kuongeza kiwango cha biashara hadi...

error: Content is protected !!