Friday , 29 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Mitaa 222 Dodoma kuboreshwa kwa anuani za makazi
Habari Mchanganyiko

Mitaa 222 Dodoma kuboreshwa kwa anuani za makazi

Mratibu wa mfumo wa uwekaji anwani za makazi Jiji la Dodoma, Joseph Nkuba
Spread the love

 

KATIKA uboreshaji na urahisishaji wa huduma katika jiji la Dodoma jumla ya mitaa 222 iliyopo ndani ya kata 41 za halmashauri ya Jiji la Dodoma inatarajiwa kupewa huduma za anuani ya makazi. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Huduma hiyo itawezesha urahisi kwa jamii kupatiwa huduma mbalimbali za kibinadamu kwa haraka na kuondosha utumiaji wa muda mwingi katika kupata huduma kama vile vifurushi na mizigo mbalimbali kutoka posta au sehemu yoyote ile.

Pia kuwekewa anwani za makazi itarahisisha utoaji wa huduma mbalimbali za kimaendeleo ya kiuchumi kwa taifa na mtu binafsi.

Mratibu wa mfumo wa uwekaji anwani za makazi Jiji la Dodoma, Joseph Nkuba amesema hayo leo tarehe 15 Februari mwaka huu alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa.

Nkuba amesema mitaa hiyo itakayowekewa itaongeza ufanisi kwenye mitaa mbalimbali katika kufikisha bidhaa na kuzuia upotevu wa mizigo ambayo uhagizwa na wananchi sambamba na kurahinzisha utambuzi wa makazi yao.

Pia itasaidia kutunza hifadhi data ya anwani yenye taarifa za makazi na postikodi ili zitumike na watu walioidhinishwa na mamlaka ya mawasiliano.

Ametaja faida zingine kwenye anwani hizo za makazi pia kurahisisha huduma za ulinzi na usalama, kuongeza ufanisi katika usimamizi wa makazi ya watu na kutambua mali na upatikanaji wa takwimu mbalimbali.

Zingine ni kuongeza tija na ufanisi katika huduma za uokoaji wa maafa, kuwezesha ukusanyaji wa kodi mbalimbali kwa urahisi na kwa wakati ikiwa na pamoja na kupambana na uhalifu katika kupata taarifa za uhamiaji na shughuli za utalii.

“Uwekaji wa anwani ya makazi ulianza zoezi lake tarehe 13 Disemba, 2021 kwa ajili ya kutambua mipaka ya mitaa 153 na hadi sasa iliyobaki ni mitaa 69 na itakamilishwa ifikapo mei 22 mwaka huu.

“Pia zoezi hilo Jiji linatarajia kuajiri vijana 100 wenye sifa ikiwemo ya elimu ya kidato cha nne,wataalam wa kutumia kompyuta na wale wenye uwezo wa usomaji wa ramani ambapo watafanya kazi hiyo kwa siku 45” amesema.

Aidha, Mratibu huyo ametoa tahadhari kwa wananchi kutoliona zoezi hilo la uwekaji wa anwani kulihusisha na upimaji wa viwanja, badala yake wawe na ushirikiano kwa serikali kwenye kipindi cha utoaji huduma za jamii ili liweze kukamilika kwa wakati.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga kuongoza usambazaji wa mitungi ya gesi 10,000 ya Taifa Gas

Spread the loveNaibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga ameahidi kuongoza kwa ufanisi...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyabiashara, wawekezaji China waridhia kuwekeza bil. 800 katika sekta 5 nchini

Spread the loveUJUMBE wa wafanyabiashara na wawekezaji wakubwa kutoka Jimbo la Changzhou...

Habari Mchanganyiko

Bil. 4.42 kumaliza uhaba maji kata 2 Musoma Vijijini

Spread the loveWANANCHI wa kata za Busambara na Kiriba, Jimbo la Musoma...

error: Content is protected !!