August 10, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Tamasha la utamaduni kufanyika Dar

Kijiji cha Makumbusho

Spread the love

KAMPUNI ya masoko inayojishughulisha na ushauri na mikakati kwa wateja ZECHY Afrika imeandaa tamasha la kusheherekea utamaduni wa mtanzania (Chemichemi Canival) litakalofanyika mwezi Septemba katika kijiji cha Makumbusho jijini Dar Es Salaam, anaandika Jovina Patrick.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Lena Kimani mratibu wa tamasha amesema: “Tamasha la chemichemi linatarajia kuzinduliwa kwa kusherehekea utamaduni wa Mtanzania. Kuna matamasha mengi nchini lakini hili linalenga kusherehekea utamaduni wetu.”

Akiendelea kuongea amesema kwamba wameona uhitaji wa kufanya tamasha hilo ili kuwasaidia wanaoishi mjini kuzifahamu na kujifunza kwa ukaribu tamaduni zao kwani wengi wao hawana ukaribu na vijijini wanakotoka hali inayofamya vijana kuwa na maana hasi kuhusu utamaduni wao.

“kutokana na utandawazi mwenendo wa maisha ya watanzania wanaoishi mjini wemgi wao hawana ukaribu na vijijini wanakotoka na hili limefanya vijana wengi wa sasa kuwa na nana hasi kuhusu utamaduni wao,” anasema Lena.

Zech wanasema kuwa tamasha hilo litafanyika mara mbili kwa mwaka na hakutakuwa na kiingilio chochote ila wametoa wito kwa watakao hudhulia kuvalia nguo zao za asili.

error: Content is protected !!