Thursday , 23 March 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Mfanyabiashara amshikia kisu mwanafunzi ambaka
Habari Mchanganyiko

Mfanyabiashara amshikia kisu mwanafunzi ambaka

Spread the love

MFANYABIASHARA maarufu katika mtaa wa Swaswa kata ya Ipagala Manispaa ya Dodoma, Charles Kalinga mwenye umri wa miaka 43 amenusurika kifo baada ya wakazi wa mtaa huo kumshushia kipigo kwa tuhuma za kumbaka mwanafunzi wa kidato cha nne mwenye umri wa miaka 17, anaandika Dany Tibason.

Mwanafunzi huyo anasoma katika shule ya sekondari Dodoma na tukio hilo lilitokea juzi saa moja usiku baada ya mtoto huyo kusikika akipiga kelele akiwa katika Pagale.

Baada ya kelele hizo mama wa mtoto huyo pamoja na majirani walienda na kumkuta mtuhumiwa akiwa amemlalia mtoto huyo akiwa tayari amesha muingilia kimwili.

“Nilianza kusikia kelele nikisikia sauti ya mwanangu akilia huku akisema mama nakufa na sauti zilikuwa zikitokea katika pagare nilipofika hapo nilimuona Charles akiwa amemlalia mwanangu huku akiwa tayari ameisha muingilia kimwili” alisema mama wa mtoto.

Akizungumza na waandishi wa habari mama wa mtoto akiwa hospitali ya mkoa alipokuwa amelazwa mtoto aliyebakwa,(Emy Mtunya) alisema mtoto huyo alitoka shuleni na kufika nyumbani ambapo alimuomba mama yake hela kwenda dukani kununua mahitaji.

“Wakati huo mtuhumiwa alikuwa kavua suruali na mwanangu akiwa anavuja damu sehemu zake za siri baada ya kumlazimisha kufanya tendo hilo.

Amesema baada ya mtoto wake kupiga kelele kwa lengo la kutaka msaada zaidi mtuhumiwa alikuwa akimuomba asiendelee kupiga kelele na kudai kuwa angempatia Sh. 100,000 ili aweze kukimbia.

Aliongeza kuwa akiwa anajitahidi kunusuru maisha ya mwanae wananchi wenye hasira kali walitokea na kuanza kumpiga mtuhumiwa kwa kipigo kikali na wengine kutoa taarifa polisi ili kunusuru maisha yake.

“Wakati naendelea na harakati za kunusuru maisha ya mwanangu wananchi wenye hasira kali walifika nyumbani na kuanza kumpiga, Kalinga kwa kila aina ya kipigo huku watu wengine wakipiga simu polisi ,” alisema mama wa mtoto.

Akizungumza wa mwaandishi wa habari mtoto aliyebakwa akiwa hospitalini akipatiwa matibanu alisema kuwa alibakwa na mtuhumiwa huyo kwa kumlazimisha huku akiwa amemshikia kisu na kumtishia kumuua iwapo atapiga kelele.

Mwenyekiti wa mtaa wa Swaswa Robert Magelanga alikiri kupokea taarifa za tukio la mtuhumiwa kumbaka mwanafunzi huyo na kutoa taarifa polisi na kushikiliwa.

Naye kaimu Mganga mfawidhi wa hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Dodoma, Caroline Damiani alisema majira ya jioni walimpokea Charles Kalinga akiwa amepigwa na alilazwa wodi namba moja na kuruhusiwa baada ya kupata nafuu na anaendelea vizuri.

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma,Lazaro Mambosasa amethibitisha kutokea Kwa tukio hilo.

Amesema mtuhumiwa huyo mpaka sasa amekamatwa na jeshi la polisi kutokana na kuwepo kwa tuhuma za ubakaji.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

NMB yamwaga mamilioni kuimarisha afya, elimu katika Kanda ya Kati

Spread the loveBENKI ya NMB imetoa msaada vifaa mbalimbali kwa sekta za...

Habari Mchanganyiko

Mwanamke afariki akifanya mapenzi kichakani

Spread the love  Mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 37 anakabiliwa na...

Habari Mchanganyiko

Taasisi ya kuendeleza uchimbaji mdogo imetakiwa kushirikiana na serikali

Spread the love  KAMISHNA wa Madini Dk. AbdulRahman Mwanga ameitaka Taasisi ya...

Habari Mchanganyiko

Almasi inayozalishwa maabara yatajwa tishio jipya kwa nchi zinazozalisha madini hayo

Spread the love  KATIBU Mkuu Wizara ya Madini Kheri Mahimbali amekabidhi rasmi...

error: Content is protected !!