August 10, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Maonyesho ya vyuo vikuu yafunguliwa Dar

Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu (mwenye suti ya bluu) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa TCU

Spread the love

WAZIRI Mkuu, Kasimu Majaliwa leo amefungua rasmi maonyesho ya 12 ya vyuo vikuu hapa nchini, anaandika Victoria Chance.

Maonyesho hayo ya siku tatu yanafanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na wanafunzi, wafanyakazi wa vyuo vikuu pamoja na wananchi waliohudhuria maonyesho hayo, Majaliwa alisema yanasaidia kujua masuala mbalimbali yanayohusu elimu ya juu.

Katika maonyesho hayo ya 12, Tume ya Vyuo Vikuu Nchini (TCU), imevitaka baadhi ya vyuo hapa nchini kusimamisha baadhi ya masomo.

Akizungumza na MwanaHALISI Online, mmoja wa wakufumzi katika banda la Chuo Kikuu cha Dar es salaam, amesema baadhi ya masomo yamesitishwa kutokana na kutokuwa na ulazima masomo hayo kuwepo katika chuo husika.

error: Content is protected !!