Saturday , 13 April 2024
Home Kitengo Michezo SportPesa yaikutanisha Simba na Sevilla
Michezo

SportPesa yaikutanisha Simba na Sevilla

Spread the love

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imetegua kitendawili cha nani atakayecheza na timu ya Sevilla ya Hispania iliyoalikwa kuja kucheza na timu mojawapo nchini inayodhaminiwa na SportPesa. Anaripoti Faki Sosi …(endelea).

Akizungumza na waandishi wa Habari leo tarehe 30 Aprili mwaka 2019 Wilfred Kidau, Katibu Mkuu wa (TFF) amesema kuwa SportPesa imefikisha mezani rai ya kuzichezesha Simba na Yanga ili mshindi acheze na Klabu hiyo iliyoalikwa kutoka nchini Hispania.

Kidau amesema kulingana na ufinyu wa ratiba ya Ligi Kuu Tanzania Bara wameamua timu ya Simba ndiyo itakayocheza na Sevilla.

Amesema kuwa uamuzi huo ni zao la majadiliano yao na  SportPesa ambapo tayari utararibu wa mchezo huo ushapangwa.

Abass Tarimba, Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji wa SportPesa amesema kuwa mchezo huo utakaochezwa tarehe 23 Mei, 2019 kati ya Simba na Sevilla ni fursa kwa Tanzania na klabu hiyo kujionesha kimataifa.

Amesema kuwa mechi hiyo itarushwa kwa matangazo ya moja kwa moja na televisheni kubwa duniani hiyo ni kutokana na ukubwa na timu ya Sevilla.

Amesema kuwa sasa ni wakati kwa Tanzania na Serikali kuitangaza nchi kwenye sekta ya utalii licha ya kuweka wazi kuwa tayari washafanya mazungumzo na Waziri wa Maliasili na Utalii, Hamis Kigwangalah kuhusu utayarishaji wa mazingira ya kitangaza nchi kwenye sekta ya utalii.

Amesema kuwa matokeo Everton kufika nchini yalionekana baada ya mchezo ule wachezaji nyota wengi kama David Beckham walifika nchini kwa ajili ya kufanya utalii.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Usiku wa Ulaya kinawak tena leo

Spread the love  LIGI ya mabingwa barani ulaya itaendelea tena leo ambapo...

Michezo

Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya ni Usiku wa Kisasi

Spread the love  LEO utarejea ule usiku pendwa kabisa kwa mashabiki wa...

BurudikaMichezo

Kizz Daniel aunguruma na EP mpya ‘Thankz alot’

Spread the loveMKALI wa muziki nchini Nigeria, Kizz Daniel ametoa EP yake...

MichezoTangulizi

Samia aipa tano Yanga

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan ameipongeza Klabu ya Yanga licha ya...

error: Content is protected !!